
Na Harid Mkali
mkali@live.co.uk
“Mwandishi katika kujibu Swali kuchangia hoja kuhusu uwekezaji na Mikopo, kuhusu mradi wa bandari ya Bagamoyo”
swali: “Kwani hawa wachina na Oman ni wawekezaji au tumeomba mkopo?”
Mimi nafikiri tusibabaishwe sana na misamiati (semantics) ya “lobbyists”. Ukweli ni kwamba baadhi ya wekezaji na mikopo ni kitu kimoja. Tena wakati mwingine utakuta matokeo ya uwekezaji yanakuwa ni: “…. far more insidious than straight loans to the host country.
Kihistoria wachumi walikuwa wanafundisha kuwa kukopesha mataifa siyo kitu kizuri, kwa kiingereza walitumia neno: risky.
Na sababu ni kwamba kuna sheria ya Kimataifa inayozuia mdai yoyote ambaye amekopesha Taifa kukamata mali za Taifa hilo kwa sababu ya deni kutolipwa.
Na hiyo ndiyo sababu hivi wakopeshaji wanalazimisha mataifa yanayokopeshwa kusaini kitu kinachokwenda kwa jina la “bilateral agreement” zinazoidhinisha wakopeshaji kukamata raslimali za Taifa linalokopeshwa kufidia deni lisipolipwa.
1) Miaka ya 1970s baada ya bei ya mafuta kupandishwa, nchi nyingi za Uarabuni zilijikuta zina pesa nyingi sana.
Nyingi ya fedha hizo zilihifadhiwa kwenye mabenki ya nchi za Kaskazini.
Kutokana na kanuni ya kiislamu inayokataza riba (interests) hizi benki za Kaskazini ghafla zilijikuta zina utajiri ambao hawakujua jinsi ya kuutumia.
Baada ya tafakuri wakaja na kitu walichokiita “recycling” yaani hizi ‘surplus money” walizokuwa nazo (kutokana na nchi za kiislamu kutodai riba) kukopesha hizo fedha mataifa ya Dunia ya Tatu.
2) Hii ndio iliyozua tatizo la madeni miaka ya 1970s na 80s yaliyosababishwa na :”over lending”. Mabenki hayakuzingatia uwezo wa hizi nchi kulipa madeni yao.
3) Wasomi wenye vichwa vyenye kujitegemea walipotahadharisha kuhusu huu ukopeshaji holela; hivi ndivyo walivyojibiwa kupitia aliyekuwa meneja wa City Bank, Walter Wriston zama hizo alipokuwa Lausanne, kwenye World Economic Forum, Switzerland, mwaka 1981:
“Bankruptcy is a procedure developed in Western law to forgive the obligation of a person or a company that owes more than it has. Any country, however badly off, will ‘”own” more than it “owes”. Countries simply could not go bankrupt; countries did not disappear; even if they occasionally had some short-term cash-flow difficulties, the cure would be ‘sound programmes’ and the time to let them work'”
In the end the debt would always be repaid because the markets would regain confidence, and it could be redeemed if only by issuing more debt.”
Ni kweli kuwa mataifa hayawezi kutoweka au kukimbia, lakini yanaweza kushindwa kulipa madeni. Ukweli huu ulipodhihirika hawa ‘International lenders’ walikuwa hawana njia ya kisheria ya kukamata raslimali ya mataifa daiwa. Hapo ndipo ‘lenders’ walipokiimbilia Benki ya Dunia na IMF – International Monetary Fund.
4) Jibu la World Bank na IMF lilikuwa ni kusambaza ‘Structural Adjustment Programmes (SAPs)’.
Lengo la SAPS halikuwa kusaidia mataifa daiwa; bali kuzuia mataifa hayo kufanya matumizi muhimu kwa wananchi wao kama vile utoaji wa elimu bure, huduma za afya bure, utowaji wa pembejeo nk ili nchi hizi ziweze kulipa madeni yao.
Huku ni kufuta uhuru wa hayo mataifa.
5) Matokeo ya masharti yaliyopo kwenye Mkataba wa bandari ya Bagamoyo na SAPS ni yaleyale.
Hivyo basi tofauti ya uwekezaji na mikopo, kwa sehemu kubwa: “… is a theoretical abstraction..”

mkali@live.co.uk.
23/09/2021.
