0 0
Read Time:1 Minute, 34 Second

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa Jijini New York Nchini Marekani leo Septemba 23,2021.

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na katibu mkuu wa umoja wa Mataifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Jijini New York Nchini Marekani Septemba 23,2021.

Rais Samia amezungumzia pia athari za mabadiliko ya Tabia Nchi na umuhimu wa kuchukua hatua za kukabiliana na janga hilo na kuyasisitiza mataifa yaliyoendelea kutimiza ahadi zao za kutoa Dola za Kimarekani bilioni 100 kwa mwaka ifikapo mwaka 2025 kama ilivyokubaliwa katika Azimio la Paris.

Wakati huo huo, Rais Samia amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Grumeti Mikael Andrea anayemuwakilisha mmiliki wa Makapuni hayo Bw. Paul Tudor Jones II ambapo amempongeza Mhe. Rais kwa kuweka mazingira bora ya biashara na uwekezaji nchini Tanzania.

Bw. Mikael Andrea amesema kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya biashara na uwekezaji nchini Tanzania, makampuni yao yataendelea kufanya kazi na Serikali ya Tanzania kwa kuongeza uwekezaji katika sekta ya utalii.

Kwa upande wake Mhe. Rais Samia amewashukuru Wawekezaji hao kwa uamuzi wao wa kuendelea kuwekeza kwenye sekta ya utalii nchini Tanzania.

Aidha. Rais Samia pia amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Antonio Guterres na kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo ulinzi na usalama barani Afrika, athari za UVIKO 19 kiuchumi na kijamii pamoja na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Rais Samia amempongeza Mhe. Guterres kwa kuchaguliwa kwa mara ya pili kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kumteua tena Bi. Amina J. Mohamed kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo.

Equity Bank ndio mdau namba moja wa Diaspora
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %