0 0
Read Time:3 Minute, 19 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Octoba 6,2021.

Naomba ieleweke kuwa haya ni maoni binafsi na wala sio msimamo wa vyombo husika!”

Mwenyekiti wa Bodi ya vyuo vya Polisi Nchini Profesa Bisanda ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Huria cha Tanzania amenukuliwa akitoa ushauri ya aina ya vijana ambao wanatakiwa kuajiriwa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama!

Lakini pia kumekuwepo na kelele nyingi kwenye mitandao ya kijamii wiki hii watu wengi wakilalamikia kitendo cha vyombo vilivyopo Wizara ya Mambo ya Ndani kuamua kuajiri vijana wenye ufaulu hafifu na kuwaacha vijana wenye ufaulu mkubwa!Kelele hizi hasa zimeelekezwa kwa jeshi la Polisi na inaokekana hata ajira katika Jeshi la Uamiaji uwenda zikafuata utaratibu huo!

Profesa Bisanda ambaye ndio Mwenyekiti wa Bodi ya vyuo vya Polisi Nchini inaonekana nae anaongoza Bodi ambayo hajui kile kinachoendelea ndani ya jeshi lake mwenyewe!

Vyombo vyetu kupitia wasemaji wake walipaswa kutoka na kuja kuweka sawa shutuma hizi kwani zinaweza kuharibu “image” hasa Mwenyekiti wa Bodi ya vyuo vya Polisi anapotoka mitandaoni na kuja kutoa ushauri wa watu wenye ufaulu upi wanapaswa kuajiriwa kwa wakati husika utadhani yeye sio sehemu ya vyombo husika!

NINI KINATOKEA KATIKA VYOMBO VYETU MPAKA VINAAMUA HIVI?

Mahitaji ya ajira katika majeshi yetu uzingatia mambo makubwa matatu wakati,mahitaji na rasilimali fedha!

1.WAKATI,Moja ya changamoto kubwa ambayo Jeshi mfano la Polisi kwa wakati huu limekuwa likipitia ni kuajiri vijana wenye ufaulu wa alama za juu ambao baada ya kupata ajira wamekuwa wakilazimisha kwenda kusoma hata wengine kusoma kwa kujificha na kuharibu ufanisi wa Jeshi letu.

Vijana hawa baada ya kunyimwa ruhusa za kwenda kusoma,wengine uamua kuacha kazi au kusoma kwa kujificha jificha!Wengine uamua kuomba ruhusa kinyemela kwa kulazimika kuingia kwenye malindo ya usiku huku mchana wakiwa masomoni kwa miaka mpaka mitatu!

Ni hatari Askari akikosa muda wa kupumzika kiasi kwamba anaweza kukosa umakini kazini hasa ukizingatia askari mara nyingi ubeba silaha ya Serikali!

Ni wazi kuwa kijana mwenye ufaulu wa daraja la nne ambao haumwezeshi kujiendeleza katika taaluma za kirai anaweza kutulia kazini na kufanya kazi zake kwa ufasaha kuliko kijana mwenye ufaulu wa daraja la kwanza au pili ambaye muda wote anawaza kwenda kujiendeleza nje ya taaluma za kipolisi!

2.MAHITAJI.Mahitaji ya majeshi yetu ubadilika kuendana na changamoto zinazojitokeza ndani ya vyombo husika!Mfano,Majeshi karibu yote uwa na programu maalum za ajira kwa ajiri ya “wataalam” wa kada mbalimbali!

Jeshi la Polisi limekuwa likitoa ajira za wataalam mbalimbali hivyo kusema kwamba polisi wanaajiri watu “viraza” tu ni upotoshaji wa kiwango cha juu!

Jeshi la Wananchi”JWTZ” pia wamekuwa wakitumia mtindo wa kuchanganya ajira za darasa la saba,kidato cha nne,sita na mara nyingine kutangaza ajira kwa wataalam tu wenye viwango vya kuanzia shahada ya kwanza mpaka shahada ya tatu wakati mwingine!Kwahiyo mahitaji kwa wakati husika ndio uamua aina ya ajira gani zitangazwe na watu gani waajiriwe!

3.RASILIMALI FEDHA,ni ukweli ulio wazi kuwa leo hii ukitangaza ajira kwa wataalam pekee yao lazima utalazimika kuwa na bajeti kubwa kuliko kuajiri darasa la saba au kidato cha nne!Mshahara wa askari wa darasa la saba hauwezi kuwa sawa na mshahara wa askari mwenye Shahada mbili!

Uwepo wa mahitaji ya askari maeneo mbalimbali ya Nchi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na kustaafu kwa askari upelekea kutangazwa kwa ajira husika lakini wakati huo huo uwezo wa Serikali kibajeti kwa maana ya jeshi pia uangaliwa!

Ieleweke tu kwamba vyombo vyetu vya ulinzi utoa ajira kwa kuzingatia mambo makubwa matatu ya hapo juu!

Ni upotoshaji wa wazi kwa Profesa tena Mkuu wa Bodi ya vyuo vya Polisi kusema kwamba kuajiri vijana wenye ufaulu mdogo kunazorotesha utendaji wa majeshi yetu kana kwamba majeshi yetu hayatoi kabisa ajira kwa vijana wasomi wa kada mbalimbali tangia yaanzishwe!

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo Cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri wa zamani Vyuo Vikuu vya Tumaini Iringa na Saut Tabora na Mtia Nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255746726484.
+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %