0 0
Read Time:4 Minute, 35 Second

mkali@live.co.uk.
08/10/2021.

Dawa za kutibu huu ugonjwa wa Uviko-19 zimekuwepo kwa muda hivi sasa – na kwa muda zimekuwa zinapigwa vita. Kwa mfano, dawa kama Covidol yetu, nyungu, na ile dawa ya Madagascar. Pia kumekuwepo na Ivermectin, hydroxychloroquine nk nk.

Lakini akina Fauci na Big Pharma walipiga vita hizi dawa zote ili kutafutia soko hivi vidonge tunavyonadiwa leo na kulazimisha chanjo zao ulimwenguni. Chanjo ambazo zimekuwa na madhara makubwa kuliko aina nyingine yoyote katika historia ya chanjo hapa duniani.

Hebu tutafakari kidogo hapa: Akina Fauci wanatangaza hivyo vidonge vyao vya kutibu uviko-19 huko Marekani; na mara tu Uingereza nayo inatangaza nchi 47 kutolewa kwenye “Red List”.
“Is it a coincidence? I very much doubt, it is.”

Sisemi dunia kufunguliwa ni kitu kibaya. La hasha. Ila umuhimu wa kuwepo kwa hizo “lock downs” ndiyo ambao haukuwepo; hasa tukizingatia kuwa hata hivi sasa huu ugonjwa bado tunao.

Fauka ya hili: je, tuna uhakika na “chemical composition” ya hivi vidonge? Isiwe yale yale tuliyoyakataa kwenye chanjo yamehamishiwa kwenye hivyo vidonge.

Wananchi wa Dunia za Tatu ni vyema kuwa na tahadhari katika mashirikiano yetu na haya Mataifa ya Kaskazini, yanayojiita yaliyoendelea. Ni kujidanganya kufikiria kuwa sisi tuna marafiki huko nje wenye kututakia afya njema, kututakia siasa na chumi zetu ziwe tulivu na imara. Marafiki wa aina hiyo hatunao. Tena katika uhusiano wa kimataifa, nchi huwa hazina rafiki.

Sisemi nchi zetu zisishirikiane na mataifa ya nje, la hasha. Lakini ushirikiano wetu uwe wa kibiashara: sisi tupate na wao wapate. Usiwe ushirikiano wa “kirafiki”, kwani kwenye biashara urafiki huwa haupo kama ambavyo nchi huwa hazina marafiki.

Kweli za kuzingatia.

1) Kweli ya kuwa nchi yetu na zingine nyingi za Afrika zimekuwa na matatizo ya mikataba lukuki mibovu, mikataba ambayo haikuwa ya manufaa kwa nchi husika, basi hii ni moja ya ushahidi wa kwamba hakuna urafiki katika biashara.

Ni nchi gani au taasisi gani “rafiki” itaweza kutuingiza kwenye mikataba ya hovyo? Au pengine hata kuhonga baadhi ya Viongozi wetu ili wakubali mikataba isiyo na tija?

2) Kadhalika kweli ya kuwa badhi ya mataifa yetu yaliwahi kupelekewa chanjo, zilizodaiwa kuwa zilikuwa ni za dhidi ya ugonjwa wa “tetanus” lakini ndani zikawekwa dawa za kuzuia au na kuharibu mimba, nao pia ni ushahidi unaoonyesha kuwa dhana ya kwamba tuna marafiki wenye nia njema na sisi huko nje ni kujidanganya.

Mathalani, miaka michache iliyopita Kenya iliwahi kupelekewa hizo chanjo ambazo zilikuwa “laced” na dawa yenye kuua uzazi iitwayo: human chorionic gonadotropin au HCG. Na mtengenezaji wa HCG ni World Health Organisation (WHO).

Viongozi wa Kenya walilaghaiwa wazikubali hizi chanjo ambazo walichanjwa wanawake tu wa umri wa uzazi (yaani miaka kati ya 14 na 49) – ingawa hata wanaume huumwa huu ugonjwa wa tetanus. Je, hapo kuna dalili ya nia njema au urafiki na waliosukumia hizo chanjo Kenya?

3) Hivi sasa kuna mbegu za mahindi ambazo tayari zimekuwa “commercialised” – yaani zinauzwa duniani kote na kampuni za Monsanto na Dupont. Mbegu hizi zinaitwa za kisasa au za uhandisi jeni/ GMO – Genetically Modified Organism.

Kwenye hizo mbegu zimewekwa kinasaba kinachoitwa “epicyte” (epicyte gene). Kazi ya hiki kinasaba ni kuwafanya watu watakaopanda hizi mbegu na kula mavuno yake wasizae milele. Yaani mwanaume yoyote akila mazao ya hizi mbegu mwili wake unatengeneza “antibodies” zitakazo athiri manii zake mwenyewe na kumfanya asizae milele. Aidha mwanamke mwenyewe kula chochote kilichotokana hizi mbegu, mwili wake naye unategeneza “antibodies” zenye kushambulia na kuua mbegu zote za kiume zinazoingia mwilini mwake na kumfanya awe mgumba daima. Tendo la ndoa litafanyika kama kawaida, lakini hakuna kuzaa.

Wanaofahamu ni mbegu zipi zina hicho kinasaba cha epicyte na ziuziwe nchi zipi, ni Monsanto na DuPont. Kwa maneno mengine ulimwengu umekuwa ni mateka.

*4). Lakini hawa watovu wa ustaarabu hawakuishia hapo. Hivi sasa, huu ugumba na uhanithi (utasa) uliowekwa kwenye kinasaba cha “epicyte” umekuwa “fine tuned” ili uathiri watu weusi peke yao. Na hii siyo “science fiction” bali ni “scientific reality” hivi leo. Nini lengo la ku-“develop” teknolojia hii, kama si: “… to wipe out the black race from the human gene pool?” Hawa ni mabeberu ambao hawataki kuona kuwepo kwa watu weusi hapa duniani. Hivyo basi tunapojipendeza kwao wanatuona kama vinyago tu sisi.

Je, taasisi na Serikali zinazofanya mambo ya kinyama kama haya tunaweza kusema ni rafiki kwa watu weusi?

Hitimisho:

Kweli ambayo kila kiongozi wa Afrika inabidi kuizingatia kwa juhudi zote ni kwamba uhusiano wetu na mataifa ya nje unategemea maslahi ya pamoja (mutual interests), siyo kupendana wala urafiki. Na hakuna sababu ya sisi kujipendekeza kwao au wao kujipendeza kwetu. Uhusiano uwe wa utegemeano wa kibiashara.

Afrika tunahitaji kununua bidhaa za viwanda (industrial goods) toka nje, bidhaa ambazo sisi wenyewe hatujaanza kuzitengeneza kama vile magari, matrekta, ndege nk.

Na hizo nchi zilizoendelea zinahitaji kununua kutoka Afrika madini ambayo wao hawana; na maendeleo yao hayawezi kuwa kamili bila ya hayo madini yetu.
Kwa mfano, haiwezekani kutengeneza injini ya ndege bila madini inayoitwa “cobalt”. Marekani hawana hiyo cobalt; lakini asilimia 80 ya cobalt duniani ipo Democratic Republic of Congo (DRC) barani Afrika.
Huo ni mfano mmoja. Afrika ina utajiri wa madini kuliko bara lingine lolote. Aidha asilimia 60 ya ardhi ya kilimo katika dunia ipo Afrika; na kila zao ambalo linafahamika na bindamu linaweza kulimwa Afrika. Tuna maziwa na mito kadha wa kadha yenye maji safi “fresh water”.

Hivi sasa Afrika inahitaji sana Marais wa aina ya hayati Dr.John Pombe Joseph Magufuli (JPM).Viongozi wenye kuamini kuwa Afrika ni tajiri, Afrika inaweza kujijenga na kujitegemea pamoja na uthubutu/ushujaa wa kuishi hiyo imani. Vinginevyo Afrika itabaki tegemezi daima.

mkali@live.co.uk.
08/10/2021.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %