0 0
Read Time:3 Minute, 36 Second

NAOMBA KUELEWESHWA SUALA LA NDEGE YA WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI YA TANZANIA BARA KUPOKELEWA ZANZIBAR.

ZAA = Zanzibar
TAA = Tanzania BARA

Naomba kueleweshwa kwa Uhuru wa mawazo “the right to express my opinion under Article 18 of the Constitution of Tanzania of 1977” kuanzia zamani hakuna pa kuongelea hadi zama za G55 ,Mchungaji Mtikila na sasa kwenye social media utapata mengi kuhusu malalamiko ya watanzania bara.
Tafuta habari ya ndege kupokelewa Zanzibar kisha soma maoni au nenda kwenye Political platforms mbalimbali,

Hoja sio MATUMIZI
Bali swala la Ujenzi na uchukuzi sio la MUUNGANO
Kwanini swala sio la MUUNGANO likafanyike Zanzibar??
Lini swala lisilo la MUUNGANO la Zanzibar litafanyika Tanzania BARA??
Ukiondoa Waziri wa Ndani Ulinzi Nje hakuna Waziri mwingine yeyote anahusika na chochote kule Zanzibar.

Pia TGFA na ATCL hawahusiki lolote kule Zanzibar sababu wapo Chini ya Wizara ya Ujenzi na uchukuzi isiyo ya MUUNGANO
Hapa MAMLAKA za Viwanja vya ndege Zanzibar wanayo yao
Usajili wa vyombo VYA usafiri wao
Kila kitu cha Ujenzi na uchukuzi chao wao wenyewe pekee DAIMA DUMU,

Ni vizuri wajue kuwa hizo ndege ni za Wizara ya Ujenzi na uchukuzi ya Tanzania BARA huko Zanzibar ni MAPOKEZI tu
Wasije anza sema SMZ imenunua ndege hizo.👇🏿👇🏿👇🏿

HUU NDIO MWISHO WA KUFIKILIA KWA VIJANA WA CHADEMA?👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Octoba 8,2021.

Ukitaka kupima ni kwa kiasi gani Taifa lolote duniani linaweza kupata maendeleo ya haraka basi angalia japo aina ya mawazo,ndoto na maono ya vijana katika Taifa husika.

Leo katika pitapita zangu kwenye mitandao ya kijamii nimekutana na mijadala ya hovyo kabisa lakini kubwa ni suala la kuhoji uhalali wa ndege za ATCL kupokelewa Zanzibar kwa hoja kwamba ndege hizo ni za Wizara ya Ujenzi ya Tanzania na si Ndege za Muungano!Aibu kabisa!

Hawa ndio vijana wa Chadema ambao wanataka tuwaachie Tanzania kesho ili waiongoze!Nilitegemea vijana hawa wa CDM wangekuwa chachu ya mawazo mbadala lakini wanaishia katika kujadili “petty issues” kwenye mitandao ya kijamii na kisambaza duniani!

Bahati mbaya sana vijana wa CCM nao wamelala baada ya kukosa teuzi za uded na udc!Akili za vijana wa CCM pia zinawaza teuzi na chaguzi tu kila siku!Hii pia ni aibu kwenu!Hivi mnataka Mama Samia,Mzee Pinda na Kaka yangu Comred Chongolo ndio wajibu hoja hizo hapo juu?wajibu wenu ni upi kwa CCM kama sio kujibu hoja kwa “facts?”.

Kwanza nianze kwa kusema kuwa ni aibu kubwa kwa Kijana wa karne hii kuwaza katika viwango hivi vya chini kabisa!Kwanza;

1.Zanzibar ni sehemu ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwahiyo suala la ndege zikapolewe wapi ni suala la maamuzi tu ya Viongozi wetu na haina uhusiano wowote na suala la umiliki wa ndege husika!

2.Ni upotoshaji mkubwa kuziita Ndege hizi kuwa ni ndege za Wizara ya Ujenzi/uchukuzi!Mtoa hoja anasema Ndege hizi ni za Wizara ya uchukuzi hivyo kuzipeleka Zanzibar ambako kuna Wizara ya uchukuzi pia ni makosa!

Kwanza sio kweli kuwa ndege hizi ni.za Wizara ya uchukuzi bali Ndege hizi ni za Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zimekodishwa na ATCL ili kuziendesha!

3.Ni aibu Kijana wa karne hii kushabia ukanda na ukabila badala ya kulinda utaifa!Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni matokeo ya Muungano wa Nchi mbili huru mwaka 1964 yaani Tanganyika na Zanzibar!

Ni aibu kuanza kubaguana Leo baada ya miaka karibia 50 ya Muungano wetu kwa kigezo cha ndege!Ni aibu kwa Kijana wa Leo kuhoji ishu ya utanganyika na uzanzibar kwani tulishavuka huko!

Malengo ya ndege za ATCL kupokelewa Zanzibar ilikuwa katika suala zima la kudumisha Muungano wetu na wala hakuna aliyesema ndege zile ni mali ya Zanzibar au mali ya bara!Ndege zile ni Ndege za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Suala la ndege moja wapo kati zile zilizowasili leo kuitwa Zanzibar haina maana ni mali ya Zanzibar!Zingeweza kuitwa Mafya,Ukerewe,Pemba,Nyasa,Serengeti na kadhalika!

Vijana wa CDM leteni hoja nzito za kuijenga Tanzania na sio hoja hizi zinazopwaya lakini vijana wa CCM msikae tu mitandaoni mkipiga umbeya na kungojea teuzi na chaguzi ndani ya chama kwani wajibu wenu wa kuipigania CCM na Taifa ni wa kufa na kupona!

Mwandishi ni kada wa CCM,Ofisa zamani, Idara Habari- Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi vyuo vikuu vya Saut-Tabora na Chuo Kikuu cha Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255746726484
+255784159968

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %