Na Mwandishi wetu WU®
Rome Italy
Balozi mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchi Italy amekwisha wasili kituo chake cha kazi Rome, na tayari amesha pokelewa rasmi na serikali ya Italy baada ya kukabidhi hati maalumu kutoka kwa serikali ya Tanzania.
Wakati huo huo amepokea ugeni mkubwa wa waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Liberatus Mulamula. Mh waziri pamoja na shughuli zake za kikazi lakini pia ratiba inaonyesha atakuwa na mkutano mkubwa na diaspora wanaoishi nchini Italy siku ya jumapili tarehe 10/10/2021. Mkutano huo utafanyika katika kumbi za ubalozi.