

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Octoba 12,2021.
Mwaka 2012 niliwahi kuulizwa na mwanafunzi wangu mmoja katika darasa langu la mwaka wa kwanza katika somo la “Development Studies”.Somo la siku hiyo”lecturer” lilihusu umasikini wa bara la Afrika.
Wakati naelezea dhana nzima ya maendeleo,Mwanafunzi wangu mmoja alinyosha mkono na kuuliza,”mwalimu,hivi Afrika tumelogwa na nani?,jibu langu likawa tumelogwa na IFM,WB,ADB na mashirika mengine ya kibeberu!
Ukimsoma vizuri Prof wa uchumi nguli duniani,Nurke katika andiko dhana lake la “Vicious Cycle of Poverty” unaweza ukawa na picha nzuri ya wapi na lini waafrika tulianza kurogwa na wazungu na mashirika yao “feki” ya misaada ya fedha na maendeleo.
Bahati mbaya sana Afrika imekuwa kama vile ng’ombe ambaye hajui kwamba anapewa pumba na majani mazuri ili baadae aweze kukamuliwa vizuri maziwa mengi na mabeberu wa mashirika ya IMF,WB,USAID,JAICA na mengineyo mengi!Laiti ng’ombe Afrika angejua kwamba majani haya mazuri na matamu anayopewa hayana lengo la kumshibisha yeye bali yana lengo la kumfanya atoe maziwa mengi tu, labda angejua,angeyakimbia majani husika!
Ukifanya tafakuri ya kina unaweza ukaona jinsi mashirika ya fedha duniani ya IMF na WB yanavyotumia janga la uviko -19 duniani kuipiga fedha Afrika kupitia kile kinachoitwa mikopo ya masharti nafuu ambayo kimsingi sio mikopo ya masharti nafuu!
IMF na WB ni sawa tu wadanganyifu wengine waliopo katika mikoa mingi hapa Tanzania ambao utoa fedha kwa mali kauli au kwa kigezo cha kuacha kadi ya banki yako na password yako kwao huku wewe mkopaji ukidhani kuwa watu hawa wana nia njema na wewe lakini baadae huwa ni kilio kwako.
IMF na WB ni sawa na fremu za kukopesha fedha zilizoenea kwa sasa Tanzania nzima ambazo zimekuwa zikiwaliza Watanzania wengi mpaka Takukuru ya Afande Brigedia Mbugo ikaamua kuingilia kati”mikopo umiza”, labda tofauti kubwa kati ya wale ndugu zangu wa Mara Credit na IMF na WB ni ukubwa wa mitaji na kuongea kingereza,basi.
IFM baada ya janga la uviko- 19 duniani, wamekuja na “package” nyingi kuitongoza dunia hasa Nchi masikini kwa kuja na mikopo wanayoita mikopo ya riba nafuu kwa ajili ya kuinua uchumi wa Nchi masikini baada ya athari ya uviko-19.”Economic stimulas package”.
Ni wazi kuwa hili mashirika ya IMF na WB yaendelee kuwepo na kufanya kazi kwa kupata faida,lazima Nchi za ulimwengu wa tatu ziendelee kukumbwa na majanga kama haya ya uviko-19 na majanga mengine ya aina hiyo!
Wakati Afrika mwaka jana 2020, ikipambana na uviko -19 kwa kusisitiza kuwepo wa “lockdown”,maofisa wa IMF na WB walikuwa wamejifungia magorofani kuchora ramani ya jinsi ya “kuipiga” Afrika kupitia mikopo yaani “stimulas package” baada ya janga la uviko -19 kuisha!
April,2020 tayari Mkurugenzi Mkuu wa IMF,Kristalina Georgieva katika kikao ramani chake na banki ya dunia”WB” yaani IMF/WB Annual Meetings wanasema;
“…the global economy is former footing as milion of people benefit from vaccine….strong policy and financial support is needed….”.
Unashangaa,je,kuanzia lini IMF na WB wakawa na maslahi na chanjo ya uviko 19?,je,WHO wapo wapi na wanafanya nini?Kwanini IMF na Ndugu yake WB waliingia kwenye mjadala wa afya hasa chanjo?wana maslahi gani na chanjo?

Miongoni mwa ramani zilizochorwa vizuri kwenye magorofa ya IMF na WB kwa ajili ya kuikamua dunia hasa bara la Afrika ikiwa “target” ni kupitia “Emergency Financing through Rapid credit Facility” yaani hii ni sawa na mikopo ya fasta ya “mara credit”ambayo hapa kwetu inatuliza kila siku!
Mingine ni “Grants for debt relief,calls for bilateral debts relief ambapo Nchi za Afrika “upigwa sound” na mabeberu kwamba zimesamehewa kulipa madeni yao ya nyuma kwa muda baada ya wakopeshaji ambao kimsingi ni “IMF na WB” kukaa pamoja na kuona kuwa Nchi masikini haziwezi kulipa madeni yao ya nyuma kwa sasa kutokana na athari za uviko-19 wakati huo huo IFM na WB wakiendelea kuzitongoza Nchi za Afrika ziweze kukopa kwa ajili ya kupambana na athari za uviko- 19.
Kimsingi,madeni ya nyuma ya Afrika yanayosogezwa mbele kulipwa mkopeshaji namba moja na namba mbili ni hao hao IMF na WB,ajabu kabisa!
Afrika inahitaji akili kubwa kutoka katika minyororo hii ya IMF na WB,Afrika inahitaji nguvu ya kibara kutoka katika minyororo hii ya umasikini”a created poverty of Africa”.
Rais Paul Kagame wa Nchi ya Rwanda waliwahi kusema hivi karibuni,!Nanukuu..
“…hauwezi kulipa deni kwa kukopa marejesho…..”,Afrika ndipo ilipofikia tunahitaji tafakuri kubwa na viongozi wetu lazima wajue kuwa safari yetu ya maendeleo endelevu haitowezekana tukiendelea kuimba nyimbo za mikopo nafuu tena kutoka kwa beberu IMF na WB.

Mwandishi ni kijana wa CCM,Mkufunzi wa zamani vyuo vikuu,Ofisa wa zamani Habari- Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.
+255784159968
+255746726484








