

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Octoba 11,2021.
Wanasiasa au askari yoyote anapaswa kujua kwamba ni muhimu kumjua adui yako kabla ya kumfyatulia risasi, ni kama Rais Samia anaonekana ameiva katika hili kwani ni dhahiri kuwa Mh. Rais amekuwa bora sana katika kuutumia ukimya wake “kuwawin” wapinzani wake!
Ni muhimu kwa kiongozi wa ngazi ya kitaifa, kujua ni wakati gani wa kusema,kitu gani cha kusema na kujua sababu ya kusema unachotaka kusema
Makamanda wana msemo wao,Nanukuu,”..don’t shoot unless you’re sure you will secure the enemy elimination……”.
Ukimya huu wa Mh.Rais, Mama Samia Suluhu Hassan unampa faida kubwa kuu mbili kisiasa;kwanza(i)adui au wapinzani wake na hata wateule wake wanakuwa hawajui Mh. Rais anawaza nini kwa muda husika.Mh.Rais aliwahi kusema hivi huko nyuma kwa wateule wake,
“….muda wote nilikaa kimya nilikuwa nawasoma na mimi mnanisoma…..tulikuwa tunasomana….”.
(ii)Wangejua anawaza nini,wapinzani na wateule wa Mh.Rais wangeweza kubadili mbinu,maficho na kujiandaa kumkabili,utamaduni huu ni muhimu sana kwa mwanasiasa wa ngazi ya kitaifa kuujua!
Mwandishi nguli wa mambo ya medani duniani,kutoka Nchini China,Sun Tzu,katika kitabu chake cha “The Art of War” aliwahi kusema kuwa, ili kushinda vita katika uwanja wa medani ni lazima majenerali waweze kuwa na mbinu za ziada dhidi ya adui!
Hata kwenye siasa na katika ujenzi wa Taifa,kiongozi wa juu wa Taifa, anapaswa kutembea katika falsafa hizi hizi za mwana “military literature gulu” Sun Tzu!Jinsi tunavyopambana na maadui wa maendeleo ya Taifa ni sawa sawa na makamanda wanavyopambana na adui katika uwanja wa medani.
HIZI HAPA NI MBINU TANO AMBAZO ZITAMWEZESHA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUSAMBARATISHA NGOME ZA ADUI ZAKE MBELE YA SAFARI.
1.Sun Tzu aliwahi kusema, hili Jeshi lishinde vita yoyote ile, lazima lihakikishe kuwa kabla ya kuanzisha vita lazima liwe na uhakika wa kushinda”…enemies should only be engaged in war when you only have a clear advantages….”mwisho wa kunukuu!
Ni kama Rais Samia ameweza kucheza na sheria hii ya vita kwani hotuba yake ya jana, ilikuja katika wakati wake sahihi mbele ya Watanzania na kuwaonyesha nini alichofanya ndani ya miezi sita na nini anatarajia kufanya!
Tayari Mh Rais ana clear advantage, kwani miradi ya awamu ya tano imeendelea kujengwa kwa spidi kubwa hivyo kuwapa imani Wananchi kuwa maendeleo katika Taifa yanakuja!
2.Sun Tzu anasema katika vita ni vizuri kujua wakati sahihi wa kumshambulia adui”Time of confroting the enemy”.Ni wazi kuwa muda wa miezi sita unatosha kutoa majibu dhidi ya matatizo ya Watanzania na kuwaonyesha njia na uelekeo wa Taifa!
Ni wazi kuwa siku mia moja pekee za kukaa madarakani, hazikutosha kumpima Rais Samia na kujua maono,dhamira na tabia zake za uongozi!Ni wazi kuwa hotuba yake ya jana, imemtambulisha Mh Rais Samia kwa Watanzania kuwa yeye ni mtu wa namna gani!Kama wapinzani wa CCM walijua wamepata mchekea mwaka 2025, nadhani sasa ujumbe umefika kwao!
3.Moja ya sifa kubwa kwangu, ambayo inampa Rais Samia utofauti na Marais wengine wa Tanzania walipita ni matumizi yake ya mbinu zita inayoitwa “Deception”.Mh Rais Samia Suluhu Hassan unaweza kumuona kwamba hawezi kuwa na madhara kwa wateule na wapinzani wake wakati kimsingi ana madhara makubwa!
Rais Samia aliwahi kusema”….mimi ntaongea kwa karamu tu…..nendeni kafanyeni kazi…jicho langu mjue linawaona…..”.
Sun Tzu anasema,hili uweze “kumpin” vizuri adui ni lazima ujue haya, Nanukuu kwa kingereza,”…when we are to attach,we must be seen unable,when we are near,we should make the enemy believe we are far away,when we are far away,we must make him believe we are near……”.
Ni ngumu kumjua kwamba, Mama Samia atafanya nini kwa wakati gani na hii imewafanya wateule wake kudhani Mh Rais hana madhara kwao lakini madhara yake wataendelea kuyaona mbeleni!
4.Moja ya njia nzuri ya kubadili upepo wa kisiasa ni kwa mwanasiasa kuwa na “political meneuver plan”!
Mh.Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kusisitiza kuwa bado anatembea katika maono,dhamira na mikakati ya hayati John Pombe Joseph Magufuli na hii inaenda kuuwa kabisa kale kakikundi kalikokuwa kanataka kumtumia hayati John Magufuli kama daraja la kutafuta uhalali kwa Wananchi”political legitimacy lobby”.
Rais Samia Hassan amenukuliwa jana akisema,”…viatu vya JPM ni vikubwa sana….lakini tunaendelea kuhakikisha tunatekeleza miradi yote aliyoanzisha na kubuni miradi mipyaa….”.
Kuanzia sasa Wananchi wa tanzania wamesikia msimamo wa Rais wao, hivyo kuanzia sasa inaweza kuwa ngumu kwa wanaotaka kutumia kivuli cha hayati JPM kutafuta madaraka kuelekea 2025.
5.Sifa nyingine ya Mh Rais Samia Hassan ni uwezo wake wa kufanya mambo yake kwa kustukiza”suprise”.Political suprise ni uwezo wa kumtengenezea adui yako “shock & confusion” ndani ya muda mfupi!
Baada ya Serikali kutangaza kuingizwa kwa chanjo ya uviko-19 Nchini, baadhi ya wanaCCM aliidaka ajenda hii na kuanza kuamasisha watu kutochanja na zaidi wakatishia kujivua Ubunge kama chanjo hiyo ingetangazwa ya lazima na Serikali
Propaganda hiyo iliweza kusambaa Nchi nzima kwa malengo ya kisiasa!Wakati wapinzani wa Mama Samia, wakijua kuwa Serikali yake inaenda kulazimisha Watanzania kuhusu kuchanja,Rais Samia Suluhu Hassan akakwepa mtego huo kwa kutangaza hiari katika kupata chanjo ya uviko!
Kwahiyo wale wote waliojipanga kutumia mtego wa chanjo kupata “political maleage” wakashikwa na kwenye “suprise” kubwa!Ilisemekana pia kuwa, uwenda Mh. Rais Samia, angetumia hotuba yake ya jana kutangaza ulazima katika kuchanja, lakini wapi!Rais kasimamia katika dhana ya kutoa elimu kabla ya mtu mwenyewe kuamua kuchanja!
Ni wazi kuwa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan ni Magufuli yule yule,mzalendo yule yule,mpinga uzembe yule yule,na zaidi mpinga rushwa yule yule!
Namnukuu,”…kama mnataka kuona rangi yangu halisi, nendeni kadokoeni hizi fedha……..”
Nani alitarajia kauli hii ya “kimagufuli” jana?sio mawaziri,sio maded na sio wananchi wa Tanzania,wotee tumestukaaa!Mama Samia ni yule yule wa awamu ya tano, na CCM ni ile ile ya awamu ya tano.
Mwandishi ni kijana wa CCM,Makamu Rais wa zamani,Daruso IJMC,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,vyuo vikuu vya Chuo cha Iringa & Saut -Tabora na Mtia Nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.
+255784159968.
+255746726484.








