“WASALITI NDANI YA CCM BADO HAWAJAJIFUNZA?” “Majibu ya hoja”
Na Chakat,Hapa Kazi Tu.
Tanzania inapaswa kuwa na vyama vya siasa vinavyojitambua na vinavyojua wajibu wao katika kuleta maendeleo ya Taifa kwani siasa sio chuki wala uhasama,siasa sio udini,siasa sio Ugaidi,siasa ni usawa,siasa ni upendo na amani.
Baada ya ushindi wa Konde, CCM itakuwa imegundua kuwa kwa sasa imepoteza mvuto kwa umma,ni muda muafaka kuwa na mkakati wa chini chini kuanzisha Chama mbadala ya upinzani ili kichukue nafasi ya Chama Cha Konde, kwani CCM inaona aibu kushindwa uko Konde, na kwa mujibu wa mtazamo,Chama Cha Konde kinajiandaa vyema kwa ajili ya mwaka 2025 na kinaweka mkakati wa ushindi na nini kitafuata baada ya ushindi,
Tumesikia wataileta code 259,tumesikia wakisema wao ni nchi huru,hapa wanaelekea kwenda kuuparula Muungano,ndipo nasema CCM iandae Chama kipya Cha Upinzani kitakachokwenda kudumisha mila na desturi za Mtanzania,Chama Cha Kizalendo mfano wa CCM kitakachokwenda kulinda rasilimali za Watanzania.
Huu ni muda wa kuanzisha mkakati wa kuanzisha chama kingine cha Kizalendo sio Cha upinzani, lengo ni kuwa chama hicho kiwe mshindani wa ccm,na hata ikitokea kikaishinda ccm, basi kitaachiwa dola, lakini kitaendelea kufanya kwa Uzalendo wa ccm ya sasa iliyopoteza mvuto,
Chama kipya kiwe Chama Cha Uzalendo,ni Chama kinachounga mkono maendeleo yanayofanywa na Chama tawala, kuenzi mazuri ya chama tawala cha sasa,Chama kitakachotembea katika nyayo za Mwalimu Julius Nyerere,Chama kitakacholeta usawa kati ya tajiri na masikini,Chama kitakachoongea sauti ya Mnyonge na mnyonge akaguswa kuwa anazungumziwa matatizo yake,na baada ya muda mchache matatizo yake kutatuliwa,
Fuatilia vizuri utajua ninachokiongea,Tazama hata mitandaoni,kwa sasa kuna post nyingi za kupima upepo juu ya kuanzishwa kwa hicho chama kingine cha Kizalendo,lakini kikwazo ni muda, na mkakati ni kuhakikisha Chama iko kinakubalika na wananchi,Matarajio ni kuwa hatua hizo zikikomaze Chama kipya ili kiweze kutembea katika nyayo za Chama kilichoasisiwa na Mwalimu Julius Nyerere na kuhuishwa na Daktari John Pombe Magufuli,Kitakapoanziswa kitapigiwa debe kuwa ni chama cha kitaifa kwani hakina ukanda wala udini, Vuta subira kama hilo litafanikiwa uje uchukue mrejesho.
Kihistoria Chama Cha Konde ndio kilipewa kazi hiyo ya kuwa backup ya ccm kuelekea uchaguzi wa 2014, chama hicho kilianzishwa na genge la Maembe, Migulu,mnamo January, Napea kutoka msoga, lakini Daktari John Pombe Magufuli alipoingia madarakani 2015 aliamua kuacha mikakati yote ya gengeni ikiwemo ya kisiasa,toka wakati huo dhambarau ikapotea.Daktari John Pombe Magufuli yeye alikuwa hapambani kwa mikakati ya kisiasa, na hapo ndio ukamuona Mwami kuwa mpinzani wa kweli baada ya Chama chake Cha Konde kufinyangwa finyangwa na kutupwa kule na Mwanaume.
Kwa sasa Genge linarudi tena lakini Watanzania wameshawajua,kwamba awa si Wazalendo kitu kidogo tu kwa wazungu,sasa tukiwapa nchi si watampa mzungu,tuache utani tumpe nchi kibaraka wa mzungu,hapana bora tuanzishe Chama kingine kitakachobeba Uzalendo, Tanzania kwanza na rasilimali ziwanufaishe Watanzania,wanaojaribu kusogeza dhambarau karibu, wakisema hakitakiwi kususia uchaguzi hata kama tume ya uchaguzi sio huru. Upepo utakavyovuma ndio utaamua hicho chama kipya kianzishwe maana mipango imeshakamilika, Tatizo Chama Cha Konde kupewa nafasi hiyo limekuja kutokana na wao kuungana na Wapemba Kinyume na hapo, hata Konde wasingekuwepo.
@CHAKUBANGA#
Jicho la Uledi: WASALITI NDANI YA CCM BADO HAWAJAJIFUNZA?
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Octoba 10,2021.
Kwa wale wanaofwatilia historia ya siasa ndani ya CCM na ndani ya Tanzania,Chama cha mapinduzi hakikuanza leo kusalitiwa na kadri unavyotaka kuisaliti CCM, ndio CCM inavyokuwa na nguvu na ushawishi kwa watanzania zaidi!
Leo,nimesoma makala mkakati ambayo imekuwa ikitembea sana katika mitandao ya kijamii ikiwa na “slogan” ya hapa kazi tu ya ndugu yetu Chakat!Kiufupi makala hii imeandikwa kimkakati kutaka kuitisha CCM ya Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake ili iweze kurudisha mpira kwa kipa,nikachekaa sana!
Makala hii ya siasa mkakati imeachiwa leo kimkakati siku ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,makamu wa Rais,Rais wa Zanzibar,Waziri Mkuu na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama wapo jijini Dodoma kuzindua kampeni ya kuchanja chanjo ya uviko -19 kwa lengo la kudhoofisha kampeni ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa jina la hapa kazi tuu!”Uzalendo”.
RAMANI YA TEAM HAPA KAZI”WAZALENDO” IMECHORWA HIVI?
Matokeo ya Uchaguzi mdogo katika Jimbo la Konde Zanzibar jana, ni wazi yamewafurahisha sana wana CCM hasa “team hapa kazi tu”na wanataka kutumia “cover” hiyo kuitisha Serikali ili iweze kusitisha kampeni yake ya chanjo ya uviko -19.
Juhudi za “team hapa kazi tu” zimeanza mbali kidogo kwa “kikundi” hicho kujaribu kuipinga wazi wazi mipango ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Mpango huu wa usaliti usharatibiwa na unaendelea kuratibiwa na baadhi ya watu wa kada mbalimbali wa ngazi za juu kwa kisingizio cha uzalendo!Unawaza, hivi nani sio mzalendo?Dkt Philip Mpango, Makamu wa Rais leo sio mzalendo?Comred Philip Mangula leo sio mzalendo?,Mzee Mizengo Pinda, leo sio mzalendo?
Nataka kusema kuwa waliomtuma ndugu yangu Chakat na team yake ya hapa kazi tu, ni wazi hawana kumbukumbu nzuri katika kile walichokisema!
USALITI KAMWE HAUJAWAHI NA HAUTOWAHI KUISHINDA CCM WAKATI WOWOTE!
Najiuliza je,ukipovu huu wa wanataka kuchochea “wasaliti” huu ndani ya CCM unatoka wapi?Ni wazi kuwa jaribio la usaliti wowote ndani ya CCM halijawahi kushinda zaidi ya wasaliti kukumbwa na aibu kubwa!Nataka kurejea baadhi ya matukio hili wasaliti wajue hatima yao itakuwaje baadae;
1.Wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015,kundi kubwa la wanaccm wakiongozwa na Mh.Mzee wetu, Edward Lowassa liliamua kukiama Chama cha mapinduzi na kwenda kujiunga na Chadema lakini matokeo yao wote tunayajua!Kamwe team hapa kazi wasithubutu!
2.Aliyekuwa kada nguli wa CCM na Waziri wa mambo ya Nje,Mh. Benard Membe, aliondoka CCM na kujiunga na Chama cha ACT – Wazalendo na kupewa nafasi ya kugombea Urais mwaka 2020,kilichomkuta mnakijua na leo anataka kurudi tena CCM!
3.Matokeo ya uchaguzi katika Jimbo la Konde kule Zanzibar leo, umejibiwa na ushindi wa kishindo wa ubunge katika jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga!Vimeumana!
Ushindi wa CCM wa asilimia zaidi ya asilimia 95+ katika jimbo la Ushetu katika ukanda wa Ziwa ambapo ndiko inasemekana ndio ngome ya team hapa kazi tu,hii imeonekana kuwavuruga mno team hapa kazi tu mpaka sasa!Mipango ya kuivuruga Serikali ya awamu ya sita kwa kutumia “cover” ya John Pombe Magufuli imeonekana kugonga mwamba, labda sasa wabadili gia angani!
4.CCM imeonekana kuwa imara zaidi kila inapotikiswa na wanachama wake”Usaliti”!Mfano,mwaka 2015 baada ya Serikali ya JK kutikiswa na Mh. Edward Lowassa na kundi lake katika uchaguzi wa mwaka 2015,Serikali iliyokuja ya JPM iliweza kujipambanua zaidi hivyo kuweza kujibu matatizo ya watanzania wengi zaidi na kufanya ikubarike zaidi!
Wakati Watanzania wengi mwaka 2015, wakidhani ndio utakuwa mwisho wa CCM kushika dola kufwatia kuama kwa kundi kubwa kwenda upinzani,lakini CCM ilivuka na kuendelea kuwa imara zaidi!
5.Ni kujidanganya kudhani kuwa, makada waliokulia na kulelewa ndani ya misingi ya CCM, wanaweza kuja kuitoa CCM madarakani!Historia imeonyesha kuwa hakuna wakati wala sehemu mbinu hiyo imewahi kufanikiwa!Rejea maisha ya kisiasa ya Maalim Seif,Edward Lowassa,Wilbroad Slaa,na wengine wengi!
Napenda kuwashauri makada wa CCM”team hapa kazi tu” kuwa, jaribio lolote la usaliti ndani ya ccm kamwe haliwezi kufanikiwa zaidi linaweza likawapoteza makada hao katika uwanja wa siasa ,kwani CCM ni taasisi ndani ya taasisi!Rudisheni mpira kwa kipa mapema,hii ngoma ni nzito sana kuchezeka!
Mwandishi ni kijana wa CCM,Makamu Rais zamani,Daruso IJMC,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,vyuo vikuu vya Saut -Tabora & Chuo Kikuu Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.
+255784159968.
+255746726484.