
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Octoba 14,2021.

Dola iliyo imara haiwezi kutikiswa na matukio ya misimu kama harakati za chaguzi, kelele za media na harakati za asasi za kiraia kwani misingi wa chama dola ujengwa katika nguzo kuu tatu za kiimani na za kiitikadi!
Dola isiyoyumba uongozwa na misingi na itikadi kuu ya Chama dola kwa maana ya falsafa,maono,dhamira na hivyo matarajio ya watu wake uanza kutengenezwa ndani ya chama dola husika kupitia watu maalum”deep state”.
Chama cha siasa ambacho uishia katika kutengeneza Ilani yake ya uchaguzi na kuiachia Serikali kutekeleza Ilani hiyo bila kutoa malengo,mbinu,strategia na wakati mwingine kushindwa kutoa dira ya Taifa basi Chama hicho hakiwezi kuepuka kitu kinachoitwa “the state failure”.
Msingi wa Chama dola lazima ujengwe katika kuielekeza Serikali yako nini cha kufanya na sio Chama dola kuiomba Serikali ifanye nini!Mipango yate ya maendeleo ya Chama dola lazima ianzie kwenye Chama chenyewe na Serikali huwa ni mtekelezaji wa mipango ambayo tayari ipo mezani mwake!
Hili kuweza kujenga Chama dola imara na wajibifu lazima wanasiasa za kimkakati wajue mambo makubwa matatu ambayo ndio yanakitofautisha Chama dola na Vyama vingine vya kawaida kawaida ambavyo labda uenda vimeweza kushika dola kwa msimu mmoja tu baadae vikaondokewa madarakani;
1.IMANI,Biblia inasema imani uweza kuamisha milima na hivyo ndivyo ilivyo kwenye siasa!Chama dola lazima kiwe na imani inayoaminika kwa watu wake katika Taifa!Chama bila kuwa na imani na maono ya wazi kwa watu wake ni kazi bule!
Mfano,Chama cha Ukomunisti cha Uchina kimeweza kutengeneza imani na maono ya Taifa ya wazi na maono ya Taifa lao, yanayoweza kupimika.CPC 19th National Congress ilikuwa ndio dira ya kwanza ambayo iliweza kutofautisha Chama dola cha China na vyama dola vingine duniani kwani CPC iliweza kuwatamanisha wachina waone kesho yao kupitia ujenzi wa imani ya Taifa kwa watawala!”…make China a great again…”.
2.MATENDO,Chama dola lazima kiwe na uwezo wa kujipambanua kwa matendo yake,kauli zake na hata maisha ya viongozi wake!Chama kinachoufyata mbele ya Serikali yake wenyewe hakiwezi kushika dola kwa miaka mingi kwani hukosa kuaminiwa na watu wake katika Taifa.
Matendo hapa upimwa na sheria na jinsi sheria hizo zinavyosimamiwa na watawala kwa maslahi ya watu wengi dhidi ya wachache,wala rushwa dhidi ya waadilifu,wazembe dhidi ya wawajibikaji,wazalendo dhidi ya mafisadi,wakabila dhidi ya wataifa.
3.MATOKEO!Imani na matendo bila matokeo haitoshi kuwa na Chama dola imara kwani imani lazima ijengwe katika kuona matokeo ya maono na ndoto za Taifa kwa watu wake!Watu sio tu lazima wasikie kinachosemwa na Serikali yao lakini lazima waone nini kimefanyika,nini kinafanyika na kipi kitafanyika mbeleni”dream”.
Lazima Chama dola kiweze kuonyesha matokeo ya matamko yake,matendo yake na matunda yake kwa wapiga kura kwani bila kufanya hivyo hakiwezi kuaminiwa na kuwa Chama dola mbeleni!”temporary political propaganda”
Wakati Chama cha Ukomunisti cha Uchina kikiwaahidi wananchi wa China kuwa,China inataka kuwa Taifa kiongozi duniani,miaka ya 2010, chini ya IX Jinping,Leo hii wachina wote wanakubalina kuhusu matokeo yaliyofikiwa na Serikali ya Rais wa China ya Chama cha Ukomunisti cha Uchina.
Dunia nzima leo inajua kuwa ndani ya miaka 10 tu ijayo,China yaweza kuwa Taifa kiongozi duniani baadala ya Marekani hata wenyewe Marekani wanajua.
Je,CCM yangu kwa kiasi gani inabeba misingi ya Chama dola hivyo kukiwezesha kutawala miaka nenda rudi bila kuhofia misimu ya Uchaguzi.Kujibu swali hili tunahitaji tafakuri ya kina kidogo!
SWALI:Je,ni lini CCM iliwahi kuwafanyia “orientation” viongozi wa Serikali yake ili waweze kujua wajibu wao katika kutekeleza maono na ndoto za Taifa?
Je,ni lini CCM iliweza kuuhisha sera yake ya ujamaa na kujitegemea kuendana na wakati huu wa sasa wenye changamoto mpya na ushindaji mpya?Wachina miaka ya 2010, chini ya Mwenyekiti wa CPC na Rais wa China IX Jinping walikuja na dhana mpya ya “Socialism with Chinese characteristics” kwa lengo la kuboresha maono,dira na mikakati ya kuiwezesha CPC kuiteka dunia ndani ya miaka kadhaa ijayo!!
SWALI:Kwanini mipango sera ya maendeleo ya CCM uishia kwenye chaguzi tu”Ilani”?Je,ni lini Ilani ya CCM iliweza kufumuliwa kabla ya mwaka wa Uchaguzi baada ya kuona fursa mpya za kitaifa na kimataifa kwa lengo la kutaka kuwatamanisha zaidi Watanzania kuhusu fursa zinaweza kuzalishwa na Serikali ya CCM?
SWALI:Je,kwa mfano CCM inawaza nini tofauti na Serikali kuhusu matumizi na uendeshaji wa SGR baada ya kukamilika?Je,CCM inapaswa kuwa na strategia tofauti katika kuendesha SGR au inapaswa iunge mkono Serikali yake hata kama wataalam wa Serikali watakuja na mpango mbovu?CCM “inacomand” vipi game ya maendeleo ya Taifa zaidi ya kutoa Ilani ya Uchaguzi!
SWALI:Je,Ilani ya CCM kuainisha ujenzi wa SGR kwenye Ilani pekee yake inatosha?au ilipaswa kwenda mbele zaidi na kutumbia, CCM inataka SGR yenye kujibu maswali magumu ya maendeleo ya Taifa!
SWALI:CCM wana mkataba na wapiga kura wake je,upo wapi mkataba wa Chama na Serikali yake?Wenzetu China,Serikali inaweza kuitwa na Chama cha Ukomunisti cha China kujibu hoja mbalimbali kuhusu maendeleo ya Taifa”accountability”.Ninachohoji hapa ni je,kwanini sisi kama chama kupitia Katibu Mkuu hatuwezi kumwita DC,RC au Waziri na kumtia Jamba Jamba?Imani yetu kwa wananchi ingeweza kupanda zaidi.
SWALI:Tumewahi kuwaza kwanini Chama cha Ukomunisti cha China kina nguvu kubwa kuliko Serikali yake yenyewe?Kiufupi IX Jinping anakuwa mbogo zaidi wakati wa vikao vya “Communist Party of China” kuliko vikao vya Serikali kwani anajua kuwa injini ya ya maono ya China ya maendeleo uanzia ndani ya vikao vya Chama chenyewe!,
Chama dola lazima kiwe na sifa za ziada za kukitofautisha na vyama vingine hivyo Chama dola kamwe hakipaswi kutishwa na Chaguzi kwani kinakuwa kimegengwa katika misingi mikubwa mitatu yaani IMANI,MATENDO NA MATOKEO!
Tunatikiswa na vyama vya upinzani wakati wa uchaguzi sababu hatujawekeza katika misingi,kanuni na utamaduni wa Chama dola, wenzetu uchina wanafanya haya kwa jasho na damu!
Tunapaswa kujihoji sasa!
Mwandishi ni kijana wa CCM,Makamu Rais wa zamani Daruso-IJMC,Ofisa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa jeshi Monduli,Arusha,Mhadhiri Msaidizi Vyuo Vikuu ya Tumaini Iringa na Saut -Tabora na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.
+255784159968.
+255746726484.








