0 0
Read Time:1 Minute, 22 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Octoba 14,2021.

Wakati Mh Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kusisitiza kuwa viatu vya mtangulizi wake hayati John Pombe Joseph Magufuli ni vikubwa mno kumtosha ukweli ubaki pale pale kuwa hata Mh Ally Hassan Mwinyi,hayati Benjamini Mkapa,Jakaya Kikwete na hayati John Pombe Magufuli viatu vya Mwalimu JK Nyerere havikuwahi kuwatosha kamwe!

Lakini pamoja na Marais wote viatu vya JK Nyerere kutowatosha, kuna Rais mmoja kati ya Marais hawa wote angalau walionyesha nia ya kutaka kuvivaa “viatu” vya hayati JK Nyerere tu ili watanzania waone angalau unathubutu kuvivaa tuu.

Hayati John Pombe Magufuli japo alijua ugumu wa kuvivaa na kumtosha viatu vya JK Nyerere lakini alionyesha kitu ambacho wanasiasa wa kizazi cha sasa tukubali tukatae ndani ya muda mfupi tumeshindwa kukifanya zaidi tinaishia kumbeza bila aibu.

Huwa najiuliza,Hivi SGR,Makao Makuu Dodoma,Bwawa la Nyerere,ATCL vyote hivi haviwaogopeshi wale wote wanaomsema vibaya John Magufuli?tunatoa wapi “guards” za angalau kuinua midomo yetu na kumsema vibaya mtu huyu?

Rais wa jamhuri ya Muungano anakiri wazi kuwa viatu hivi ni vikubwa sana kwake, lakini sisi tunasema,hata yeye Magufuli viatu vya Mwalimu Nyerere havikuwahi kumtosha kabisa!

Wanachotaka kuona Watanzania ni kwamba angalau una thubutu kivivaa tu,hiyo ndio kiu yao!Tunaweza kupata ushindi wa kishindo mwaka 2025 sio kwa sababu viatu vya JPM vilitutosha hapana bali kwa sababu angalau tulithubutu kuvivaa!

Watanzania hawa wanatuangalia kwa macho yao yote “kodo” kamwe tusipuuze ukweli huu,itatugharimu!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan katika picha na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Tano Hayati Dr John Pombe Magufuli

+255784159968
+255746726484.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %