0 0
Read Time:1 Minute, 43 Second

Na Mwandishi

Josias Charles

Ni wazi kuwa Gharama za huduma ya Internet Iko juu kupita kipindi chochote kile katika historia ya Tanzania.

Inawezekana jambo hili linafanywa na Wanasiasa wanaoogopa athari ya Mitandao ya Kijamii katika Shughuri zao za Kisiasa lakini hawajui athari za kiuchumi zitokanazo na gharama ya Internet kuwa Juu.

Miaka ya 2013-2015 mtanzania alikuwa anaweza kupata Kifurushi Cha wiki Cha GB 3 Kwa Shiling 1000 ya kitanzania, GB hizi zilikuwa zikitumiwa Kwa wiki zima bila kuisha na bila mtu kuzima Data tofauti na Sasa ambao hata ukipewa GB 3 zitaisha ndani ya masaa machache.

Wajasiriamali wengi wanaotegemea huduma ya Internet kuendesha Shughuri zao za Kila siku Kwa Sasa wanafanya kazi roho juu Kwa kuhofia Bundle kukata. Kila siku watanzania wanalazimika kuunga Kifurushi Cha Wiki ambacho nacho hudumu Kwa masaa machache. Sio ajabu mtu akaunga vifurushi vya wiki mara Saba ndani ya siku 1. Hii ni nchi ambayo inahimiza matumizi ya TEHAMA kufikia maendeleo endelevu.

Kundi kubwa la Vijana ambao Serikali imeshindwa kuwaajili wameamua kuwekeza muda wao kujitafutia Fursa ndani na nje ya Nchi Kwa kutumia huduma ya Internet. Lakini bila Huruma huduma hii imekuwa ghari mno kuliko hata Bei ya mazao makubwa ya biashara.

Laiti kama Serikali yetu ingetaka kupambana na Changamoto hata za Machinga nadhani ingejikita kutoa elimu ya matumizi sahihi ya Internet maana Machinga wote wangetafuta mbinu za kuuza na kutangaza bidhaa zao online. Lakini Kwa gharama kubwa hizi za internet unadhani nani atapata nguvu hata ya kuweka Status bidhaa anazouza? Wanunuzi watanunuaje bundle kuangalia Status za Machinga wakati Bidhaa wanazotaka zinathamani ndogo kuliko gharama ya bundle?

Leo hii Machinga mliyepenga naye Chumba kimoja unaweza usijue anauza Nini kwani Hana bundle ya kutangaza bidhaa zake, na wewe unaweza kutembea kilometa 20 kufuata huduma anayouza machinga huyo huyo kutokana na kuwa hauna bundle la kuangalia bidhaa zake.

Huduma ya Internet inapaswa kuwa huduma ya Bure Kwa Taifa linalopogania kusonga mbele kama Tanzania. Ni vema wataalamu wetu wa UCHUMI kuacha kuchukulia mambo kirahisi bila kufanya tathimini ya athari ya Gharama kubwa za internet katika Ustawi wa Taifa letu.

#Freeinternet4All

Josias Charles

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %