0 0
Read Time:2 Minute, 21 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
November 4,2021.

Unaweza kusema kwa madaha kabisa kwamba karibu nyumbani Mama wa Taifa,karibu nyumbani mwana mazingira halisi, karibu nyumbani mwana sauti kwa wasio na sauti duniani,Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muu gano wa Tanzania.

Mama Samia wa Glasgow, Scotland unaweza kusema alikuwa katika dimba lake la nyumbani kwa maana ya eneo la mazingira kwani amewahi kuhudumu katika nafasi ya Waziri wa Muungano na Mazingira kwa muda.

Hapana shaka kwamba Rais wangu amethibitisha pasipo shaka kwamba anajua kuyatumia majukwaa haya ya kimataifa kwani inaonekana anajua nini la kusema,kwa nani,na kwa wakati gani!

Mwezi jana tu aliweza kuliteka jukwaa la “UNGA” pale mjini New York,Marekani baada ya kuibuka na ajenda nzito kidunia ya jinsia na kuweza kuungwa mkono duniani kote!

Jana tena, Rais wa Tanzania,Samia Hassan aliweza kuiteka dunia baada ya kuichambua na kuivaa ajenda ya mabadiliko ya tabia Nchi kwa style ya kipekee kiasi kwamba kuyafanya mataifa masikini yote duniani kuunga mkono hotuba yake!

1.Rais Samia jana alimua kuvaa gauni la Afrika na pia kuwa msemaji wa Nchi za ulimwengu wa tatu ambazo zinabeba mzigo mkubwa wa mabadiliko ya tabia ya Nchi!Anasema nanukuu.

“….sisi Tanzania na Afrika tunachukua hatua kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabia Nchi,….sasa kwa nini ninyi hamfanyi?…….”.

2.Mh Rais Samia alikwenda Glasgow na ajenda ya Uchumi wa Mataifa masikini kwa kutolea mfano wa Nchi yake Tanzania.

Kitendo cha Rais wangu kuunganisha ajenda ya mabadiliko ya tabia Nchi dhidi ya Uchumi wa Kilimo iliweza kuwastua wakubwa wengi pale Glasgow Scotland!Samia anasema,nanukuu.

“…..karibia asilimia 30 ya GDP ya Tanzania inatokana na Kilimo…kwahiyo kuharibu mazingira ni kuharibu Kilimo ambacho kinategemea mvua…..”.

Kwa kifupi Mama Samia alikuwa anataka kuwaambia wakubwa kuwa kwa kudharau ajenda ya mabadiliko ya tabia ya Nchi maana yake unatengeneza balaa la njaa katika Afrika na katika Nchi nyingi za ulimwengu wa tatu,hoja nzito sana hii!Wazungu wamestuka mno!

3.Rais Samia anasema,nanukuu hapa.

“….Kama sisi nchi masikini tunachukua hatua za kukabili mabadiliko ya tabia ya Nchi,….Kwanini ninyi msifanye…..?”.

Kwa kifupi hili ni swali nzito na Mh Rais alijenga hoja hii kupitia juhudi ambazo Serikali ya Tanzania inafanya katika kulinda mazingira na madhara ya mabadiliko ya tabia Nchi.Hii ni heshima kubwa kwa Tanzania kuliko tungeenda mikono mitupu.

Ni wazi sasa kuwa Rais wa Tanzania anaweza kuwa msemaji mkuu wa Nchi za ulimwengu tatu katika masuala ya kimataifa,Afrika inapaswa kumuona Samia Suluhu Hassan kama fursa katika majukwaa ya kimataifa hivyo waanze kumtumia kupenyeza ajenda za kimataifa kuhusu Afrika

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari – Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli,Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,vyuo vikuu vya Saut na Tumaini Iringa,na Mtia nia Ubunge Jimbo la kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %