0 0
Read Time:3 Minute, 45 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi
Kyela,Mbeya.
November 3,2021.

Maono,wivu,dira na matamanio ya Taifa lolote makini duniani yanapimwa kwa mambo makubwa matatu na katika hilo sina shaka kabisa(i)Maono ya katiba ya Taifa husika(ii)uimara wa Ilani ya Chama dola na (iii)maono ya Rais wa Nchi husika.

Kwa mtu makini akitazama mambo hayo makuu matatu basi anaweza akasimama na bila kupepesa macho, anaweza kutamka kuwa Taifa fulani linakwenda kuwa Taifa kubwa au laa!

Lakini lililo kubwa hapa zaidi ya yote kati ya uimara wa katiba,uimara wa ilani kwa maana ya Chama dola,lililo kubwa ni Uongozi maono na wenye dira isiyoyumba!

Rais wa Zanzibar,Mh. Hussein Ally Mwinyi anaibeba vizuri sifa ya tatu ndio maana sitoshanga kuiona Zanzibar ndani ya miaka yake kumi ikipaa Sana!Kwa kifupi,anayejiandaa kumrithi Hussein Mwinyi lazima aanze kujiandaa sasa kwani bila hivyo tutakuwa na kazi kubwa pale visiwani muda ukifika!

RAIS HUSSEIN ALLY MWINYI ANABEBA VIASHIRIA VYOTE VYA KUIFANYA ZANZIBAR KUWA KISIWA TISHIO NDANI YA BAHARI YA HINDI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan ampongeza Dr Mwinyi

Rais bora ni yule ambaye anaweza “kuifunika” (i)katiba na (ii)Ilani ya Chama chake mwenyewe na kufanya mambo ambayo ni “exceptional” yaani yasiyo ya kawaida!Hayati John Pombe Magufuli alikuwa na sifa hiyo lakini Rais Hussein Ally Mwinyi nadhani ndio kwa sasa, “anaivaa,anaikoga na kuinywa”sifa hiyo barani Afrika.Kwa ufupi Hussein anaweza kuwa mtu muhimu sana ndani ya CCM baadae baada ya Mama kumaliza kipindi chake 2030.

Rais wa Zanzibar,Hussein Ally Mwinyi ana sifa kuu tatu ambazo bila shaka kiongozi wa juu akiwa nazo zinakuhakikishia kuwa safari yenu kama Taifa ya kuelekea kuwa Taifa kubwa duniani”competative nation” inatimia ndani ya muda.

1.Mwinyi anaishi katika “Boss type of leadership”.Aina hii ya uongozi mara nyingi ukimbiwa sana na viongozi wengi wa afrika kwa kuogopa lawama ya kuwaumiza marafiki na watu wao wa karibu!

Katika aina hii ya uongozi Rais au kiongozi ufanya lolote bila kujali atamumiza nani “as long as it for National interests”!Hii inaitwa punda afe lakini mzigo ufike!Mara nyingi aina hii utumika pale watu unaowaongoza hawajui wapi unataka kuwapeleka kwahiyo kiongozi wa juu ulazimika kutumia”coercive means” kufikia malengo ya Taifa!

JPM na Hussein Mwinyi wameweza kuishi katika sifa hii au aina hii ya uongozi!Hongera kwa mwaka mmoja wa SMZ,kazi pale visiwani Zanzibar ni nzuri sana!

2.Mwinyi anaishi katika sifa ya pili inaitwa “Pursueder type of Leadership”.

Aina hii ya uongozi utumika pale kiongozi wa juu anapopata upinzani kuhusu ajenda yake ambayo anataka kuitekeleza ndani ya Taifa lakini bado kwa maono yake, anaona ina maslahi mapana ya Taifa ya baadae!

Pursueder uwa na uwezo wa kuaminisha watu wake kwa hoja nzito na kuwaaminisha kuwa kwa ajenda hii tunaweza kulifanya Taifa letu kuwa Taifa kubwa na tajiri.Hayati Magufuli na Hussein Mwinyi wanaishi ndani ya sifa hii!

Rais Mwinyi anasema kwa kujiamini kabisa kuwa Uchumi wa Blue kupitia bahari ndio utaenda kukifanya kisiwa cha Zanzibar kuwa kisiwa tishio na ni kama wazanzibari wengi wameamini,kazi inaendelea!

3.Rais Hussein Mwinyi pia anaishi kwenye “educator type of Leadership”.

Aina hii ya uongozi utumika pale Wananchi wako wanakuwa hawajui unataka kuwapeleka wapi lakini wewe kama kiongozi wa juu unakuwa umebeba ramani yote!Nani Zanzibar aliujua Uchumi wa Blue?Nani Zanzibar alijua uvuvi wa bahari kuu?Nani Zanzibar alijua kwamba rushwa ni adui wa haki kwa vitendo?

Rais Mwinyi ndani ya mwaka mmoja amewafanya wazanzibari waimbe wimbo mmoja tu yaani(i)uchumi wa blue,(ii)Uchumi wa bahari Kuu(iii)rushwa na ufisadi Zanzibar hapana!

Unashindwaje kuota Mzanzibari kuwa miaka kumi ijayo Zanzibar inaenda kuwa kisiwa tishio ndani ya bahari ya Hindi!Hauitaji mganga wa kienyeji kuyaona haya kwani haya tunayaona kupitia ishara hizo hapo juu!

CCM tumtunze Rais wa Zanzibar sana kwani dalili zi wazi kuwa kuna siku zinakuja atatafaa kabisa,lini?mi sijui lakini najua atatufaa Sana sana sana!

Pichani aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi (kushoto) na aliyekuwa Makamo wa Kwaza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) walipokutana Ikulu Chato mkoani Geita mnamo Januari 14,2021.

Mwandishi ni Kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Saut & Tumaini University Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %