WU®
Huenda mwimbaji wa Bongofleva kutoka WCB Wasafi, Diamond akaufunga mwaka huu kwa kishindo cha aina yake kwa sababu hadi sasa amependekezwa kuwania tuzo 18 za kimataifa.Advertisement
Huenda mwimbaji wa Bongofleva kutoka WCB Wasafi, Diamond akaufunga mwaka huu kwa kishindo cha aina yake kwa sababu hadi sasa amependekezwa kuwania tuzo 18 za kimataifa.
Mwaka huu Diamond alikuwa msanii pekee ukanda wa Afrika Mashariki kutajwa kuwania tuzo za BET 2021 katika kipengele cha Best International Act, ikiwa ni mara yake ya tatu.
Tuzo hizo kubwa duniani ambazo zilitolewa Juni 28, 2021 huko Los Angeles, Marekani, hazikumpa raha, kwani ushindi ulikwenda kwa Burna Boy wa Nigeria, ambaye aliandikisha ushindi wake wa tatu mfululizo.
By Peter Akaro