0 0
Read Time:6 Minute, 39 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Nov 17,2021.

Kwa hali ya sasa ili tuweze kuwa Taifa tajiri angalau Afrika ,hatuhitaji kuvuna rasilimali za ndani ya nchi yetu pekee yake bali tunahitaji kuwa watu wenye akili kubwa ya kuweza kutengeneza mipango mkakati ya kiuchumi ya kitaifa kupitia taasisi mtambuka kwa kutengeneza “Intergrated Nation Plans”.!

kwa maana kupitia taasisi mbalimbali kama vyombo vya ulinzi na usalama wachumi,wafanyabiashara,serikali,mabenki na wadau wengine wa ndani ili kwenda kuyafuta maslahi ya Tanzania nje ya mipaka kimkakati zaidi kupitia dhana ya “Foreign economic diplomacy & economic intelligence of Tanzania”.

Kwa sasa naona wazi kuwa mipango yetu ya kuwa Taifa kubwa na tajiri Afrika, haiwezi kufanikiwa kwa haraka”sustainable” kama tutataka kuvuna rasilimali na fursa za ndani ya nchi yetu pekee yake, twapaswa kuwa na mipango yenye sura “mbaya” ama “nzuri” katika kutafuta maslahi ya Tanzania nje ya mipaka yetu.

Lazima dhana hizi mbili kwa maana ya kuvutia wawekezaji kutoka nje kuja Tanzania kwa maana ya FDIs na dhana ya sisi kama Taifa tuweze kutoka nje ya mipaka kwenda kutafuta maslahi yetu zaidi kwenye nchi zingine dhaifu,lazima viende pamoja!

Lazima kuanzia sasa sisi kama Taifa, tunapaswa kutengeneza mpango wa kitaifa na kuyalazimisha makampuni yetu ya ndani ya nchi yaweze kutoka kwenda kutafuta fursa nje ya mipaka kwani faida zake ni kubwa kiuchumi na kiulinzi. Lazima tuwe na makampuni mengi kama ya Bakhresa yaweze kutawala masoko ya majirani zetu kwani kwa kufanya hivyo, kuna faida kubwa za kiulinzi na kiuchumi kwa upande wetu kama Taifa!

Lazima sisi kama Taifa ni lazima “economic intelligence yetu” itwambie ni wapi tunaweza kwenda kama Taifa ambako bado kuna udhaifu wa sera za kiuchumi na udhaifu wa usimamizi wa rasilimali za Taifa “Instability” ambako wafanyabiashara na Serikali tunaweza kupenya na kuvuna utajiri kwa maslahi ya Tanzania yetu ya leo na baadae.

Udhaifu wetu wa sera za kiuchumi kama Nchi, kwa miaka zaidi ya 30 nyuma ulifanya mataifa na makampuni makubwa ya kibeberu duniani, yaje kuvuna rasilimali zetu za madini na wanyama poli kupitia uwekezaji na utalii.

Na sisi kama Taifa ni wakati sahihi leo, sasa lazima tuanze kuyatafuta maeneo dhaifu duniani kwa malengo hayo hayo ya kuvuna utajiri wa mataifa mengine kupitia makampuni yetu kama Twiga Corporation na kampuni zingine za kizalendo pamoja na wafanyabiashara wengine wa kitanzania, wawezeshwe kupata mitaji na Serikali hili wakafanye kazi ya kutafuta maslahi zaidi ya Taifa katika mataifa mengine dhaifu duniani!

Rais John Pombe Magufuli aliweza kutuamsha kuhusu jinsi tulivyoibiwa rasilimali zetu kama Taifa kwa muda mrefu, kwahiyo ni wakati huu sasa wa kujiongeza na kuwaza jinsi gani na sisi tunaweza kutumia udhaifu wa Nchi nyingine duniani kwenda kutafuta maslahi ya Tanzania sasa nje ya mipaka.

Kwa mfano,Jiji la Kampala, Uganda, inasemekana ndio soko kuu la “Gold Black Market” kwa dhahabu inayotoka Congo kwahiyo ni rahisi tu kusema Uganda inanufaika na dhahabu ya Congo kuliko Congo yenyewe.Je,wafanyabiashara na makampuni ya kitanzania yakipewa mitaji na kwenda Congo kununua dhahabu hiyo kwa bei chee na kuja kuifanyia “value addition” kwenye mtambo wetu wa pale Geita na kuuza kwa bei kubwa zaidi au kuweka katika gold reserve yetu pale BOT.

Tunahitaji kuwa na “a strong economic intelligence unit” katika Balozi zetu ziweze kutusaidia kujua nchi dhaifu kisera ambazo tunaweza kwenda kuvuna utajiri wao kwa kutumia udhaifu wa sera na sheria zao.

Lazima Serikali yetu ya awamu ya sita ya Samia Hassan iwe nyuma ya mpango mkakati huu kwa kuviwezesha vitengo na idara za “economic intelligence” katika Balozi zetu na katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ili viweze kusaidia Serikali kupata taarifa sahihi za fursa za kiuchumi katika mataifa mengine kwani bila kuwa na taarifa za ndani na za uhakika hatuwezi kutekeleza dhana hii ya kwenda kutafuta na kuvuna fursa katika maeneo mengine duniani.

Tusione aibu hata siku moja kutekeleza dhana ya “primitive acculturation of wealth” kwani Nchi wenzetu mpaka sasa wanafanya katika njia za kisasa zaidi, kwa maana kufanya hivyo pekee ndio usalama wetu kama Taifa!

Unapokuwa na makampuni ya kizalendo kama Bakhresa Group of Company katika Nchi just kwanza, unajihakikishia mambo makubwa matatu; kwanza kujenga uwezo wa kushindana katika masoko mengine ya nje ya mipaka,pili kuweza kuvuna utajiri wa Nchi jirani kupitia kuuza bidhaa na huduma zako lakini la muhimu kabisa, mnaweza kutumia kampuni hizi au biashara hizi kutekeleza mipango yenu ya kiulinzi na kiusalama kama Taifa,wahusika wanajua haya!

HAYA MAMBO YANAFANYIKA DUNIANI KOTE KWA SASA!TUAMKE!

Mataifa mengi kwa sasa uunda vikosi maalum kwa ajili ya kutekeleza dhana ya “foreign economic intelligence”kwa kusoma fursa na udhaifu wa Nchi nyingine duniani na kutumia udhaifu huo kama daraja la kuvuna utajiri katika mataifa yao.

CHINA WANA “CHINA’s BELT AND ROAD INITIATIVE”.

Huu ni mpango mkakati kabambe uliobuniwa na Rais wa uchina ndugu XI Jinping kwa kuhakikisha maslahi ya China ya ndani yanaweza kupatikana nje ya mipaka ya China kwa Serikali ya Beijing kuanda mpango wa kuwawezesha makampuni ya China kwenda nje ya mipaka hasa Afrika kwa kuyapa mikopo kupitia mabanki na kuyatafutia fursa nje ya mipaka ulaya,asia na afrika.

Mwaka wa 2013, mpango huu mkakati wa China, ulitangazwa na Rais wa China Jinping na akauita “Peripheral Diplomacy work” ambapo XI Jinping alinukuliwa na nanukuu kwa Kingereza hapa.”…..China’s neighbours has extremely significant strategic value……”.anamaliza.

Angalau Rais Samia Suluhu Hassan nae anaweza kutembea kwenye dhana hii ya kuwaona majirani zetu dhaifu kama daraja muhimu katika maendeleo yetu kwa sasa kwa kuendelea kuwekeza katika ujenzi wa SGR ambayo itaweza kuwahudumia warundi,wanyarwanda na wakongo pia.

MPANGO WA “NEW FOREIGN TRADE POLICY 2021/2026” WA NCHI YA INDIA.

Wizara ya biashara na viwanda ya India kwa sasa imetengeneza mpango kabambe wa biashara ya nje wa mwaka 2021 mpaka 2026 ambao ulizinduliwa April 1,2021 wenye lengo mahususi la kulifanya Taifa la India kuwa kiongozi wa biashara ya kimataifa duniani!

Mpango huo umetengenezwa kupitia Serikali kwa kuhusisha vyombo vyote muhimu na wadau wote kutoa maoni jinsi ya kutekeleza ndoto hiyo kubwa ya Taifa la India.
Vyombo vya Ulinzi vikiwa waratibu wakuu wa mpango husika.

MCHANGO WA TAASISI MKAKATI ZA CHINA KATIKA KUTEKELEZA DHANA YA UCHUMI JASUSI DUNIANI.

Naanza kwa Kunukuu andiko moja kuhusu China.”..linked to China’s growing energy and resource acquisition in Africa,it’s ever growing intelligence operations coinciding with an increasing presence of Chinese Intelligence personnel on the Continent………..”.mwisho wa kunukuu.

Kwa kifupi wanasema uwepo wa mipango ya kiusalama ya Nchi ya China ndani ya bara la Afrika, imesaidia sana kuifanya China kuitekeka miradi mikubwa ya nishati na rasilimali nyingine katika Afrika.

Jukumu hili kubwa na la kimkakati kwa Taifa la China, uratibiwa na wizara ya Ulinzi na idara ya ujasusi wa kijeshi”DMI” pamoja na wizara ya biashara ya china “Intergrated Institutional Plans”, unaweza ukasema.

Wizara ya Ulinzi ya China ndio chombo cha kimkakati cha kuweza kulinda sekta ya viwanda ya China ndani na nje ya mipaka kupitia “Industrial Intelligence” kwa kufanya shughuli za kijasusi kwa maslahi ya viwanda vya China.

Kwa mujibu wa takwimu za UN,Nchi ya UChina ndio “Manufucturing Power House” ya dunia ikiuza asilimia 18 ya bidhaa zake zote nje ya China na viwanda vyake vikitoa ajira milioni 200+ kwa wachina.

Je,tunataka kuwa Taifa kubwa?kama jibu ni ndio lazima tuunganishe nguvu za pamoja kwa maana ya Serikali,vyombo vya ulinzi,wizara ya viwanda,mabenki,wafanyabiashara na tuanze kufikilia mipango mikubwa kwa ajili ya Maslahi ya Taifa letu Tanzania.

Mpango wetu huu wa kitaifa kwa sasa wala usilenge kushindana na Nchi kama China au Marekani kwani hatutawaweza, kwani Nchi “size” yetu zipo nyingi ndani ya Afrika hii.

Tunaweza kwani tayari tuna dereva kisiki wa kutupeleka tunakotaka,Mh Rais Samia Suluhu Hassan anaweza kuutekeleza mpango huu kwa muda mfupi na kwa umakini mkubwa!Ni suala la mda tuu,Tanzania kama Nchi tunaweza kuwa “Giant of Africa” tukiamua leo.

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa jeshi Monduli -Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Saut na Tumaini University Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %