0 0
Read Time:1 Minute, 6 Second

Na Mwandishi wetu WU®

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dr.Hussein Mwinyi akiongozana na mwenyeji wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Mhe.Mashego Dlamini, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Shaka Jijini Darban Afrika Kusini, kuhudhuria Mkutano wa ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara kwa Nchi za Afrika,utakaofanyika leo 15-11-2021 Jijini Durban.

Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasili Jijini Durban, nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki ufunguzi wa Mkutano wa Maonesho ya Biashara baina ya Nchi za Afrika, unaotarajiwa kuanza leo November 15, 2021.

Akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa King Shaka Jijini Durban, Rais Dk. Mwinyi alipokewa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mashego Dlamini, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi pamoja na Maafisa wengine wa Ubalozi pamoja na kupokewa kwa gwaride la Heshima la Nchi hiyo.

Mkutano huo ambao ni mwaliko kutoka kwa Rais wa Afrika Kusini Cyric Ramaphosa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utafuatiwa na vikao mbalimbali ambavyo vitaeleza fursa za kibiashara, masoko katika Nchi za Afrika ambapo viongozi kadhaa wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo Marais wa nchi mbali mbali za Afriika, Marais wastaafu, pamoja na Viongozi wa Mashirika ya Kimataifa.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %