

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Nov 14,2021.
Nchi yoyote makini duniani “uitisha” au uvutia wawekezaji kutoka nje angalau katika maeneo machache ya kimkakati huku ikiendelea kujijengea uwezo wake wa ndani kwa ajili ya “kutake over” miradi husika kwa maslahi ya Taifa ya baadae.
Nchi zote zenye mission pana duniani, uhutumia uwekezaji wa nje kama daraja la kufika wanapotaka kwenda kwa kuhakikisha wanatumia watu wao wa ndani “best brain”kwa kuhakikisha wanachota ujuzi wa kuendesha miradi husika na baadae Taifa kuja kutekeleza miradi yake lenyewe.
Bahati mbaya sana sisi kama Taifa,tumeamua kuutumia uwekezaji wa nje kama “ndoa” baina yetu na wawekezaji hivyo kutufanya tuendelee kufungwa na wimbo wa FDI’s miaka nenda rudi!
UWEKEZAJI TOKA NJE YA NCHI UNAWEZAJE KUTENGENEZA UCHUMI FAKE KATIKA TAIFA?
1.Uwekezaji toka Nje kwa maana ya “FDI’s” usipokuwa strategic, kuna uwezekano mkubwa wa Taifa letu kutengeneza watu masikini zaidi kuliko ya kabla ya uwekezaji wa nje kuja Nchini!
Wachumi wanajua dhana nzima ya “crowd out effect” jinsi inavyofanya kazi!Hii ina maana kwamba ukiruhusu uwekezaji katika maeneo mengi hasa yale wajasilimali wadogo wadogo wanajipatia kipato then unaenda kuuwa kabisa dhana nzima ya uwezeshaji kwa wazawa!
Mfano,Leo hii ukiruhusu mwekezaji katika sekta ya mafuta ya alzeti pale Singida maana yake utakuwa umeua wajasiliamali wa biashara husika Nchi nzima!Hivyo hivyo kwa mawese ya kule Kigoma na Kyela.Haitaji akili kubwa kujua haya!
2.Uwekezaji wa nje unaweza ukakupa “show off economy” kwa maana ya GDP kubwa hivyo tunaweza kujisifia kuwa Tanzania ina GDP kubwa kutokana na shughuli za kiuchumi kutanua!
Kwanini naongea suala la “show off economy”?,GDP ambayo angalau asilimia 70 inatokana na uwekezaji tena toka nje hiyo ni “GDP show off”.Biashara za kimataifa zina tabia ya kuamisha mitaji na faida kutoka Nchi moja kwenda nyingine!
Leo hii mgodi wa Barrick Gold kwa mfano, wakimaliza kuchimba madini yao kule kanda ya Ziwa, maana yake wataondoka na mitaji na faida zao kwenda mahali pengine duniani!Hii ina maana kuwa katika mazingira hayo, GDP ya Tanzania lazima itashuka tu!
Hapo ndipo ulipo utofauti kati ya uwekezaji kutoka nje na uwekezaji wa wazawa kwani uwekezaji wa wazawa unakupa uhakika wa kubakiza mitaji na faida ndani ya Nchi hivyo kuifanya GDP ya Nchi kuwa stable milele!Ona Salim Bakhesa alivyoweza kutanua uwekezaji wake na kuifaidisha Nchi kwa miaka zaidi ya ishirini!Hivi Salim Bakhresa ataondoka siku moja kwenda wapi?
3.Ni wazi kuwa uwekezaji wa nje utaleta ajira za haraka kwa Watanzania lakini tunaweza kujikuta tunatengeneza wafanyakazi wengi huku tukiua kabisa sekta za Kilimo,biashara,viwanda vidogo vidogo hivyo kuuwa kabisa ubunifu na teknolojia katika maeneo tajwa hapo juu!
Tunapaswa kuwaza deeply kuhusu uwekezaji na tuweke wazi ni maeneo gani tunahitaji uwekezaji kutoka nje na wapi hatutaki uwekezaji la sivyo tunaweza kujikuta tunaiingiza Nchi katika utegemezi wa milele”for life dependency”.

+255784159968.