0 0
Read Time:4 Minute, 3 Second
jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Nov 13,2021.
15:30 PM

Ni wazi kuwa Mh. Rais wangu, Mama Samia Suluhu Hassan, amekuwa akiangaika usiku na mchana”kuitisha” uwekezaji toka nje ya Tanzania kuja kuwekeza kwa ajili ya kufungua Nchi yetu kiuchumi na kufanikisha vijana wengi wanapata ajira huku Serikali ikipata kodi kwa ajili ya maendeleo ya watu wake!

Nia njema hii ya Mh Rais wetu wa Nchi inapaswa kuungwa mkono na kila mtanzania lakini pia wajibu wetu sisi vijana wa CCM ni kuhakikisha tunakuwa jicho la tatu la Serikali yetu kuhusu mipango yake yote na kuweza kuishauri Serikali yetu kwa maslahi mapana ya kiuchumi,kisiasa na kiusalama ya Nchi hii!Wajibu wetu huu hatuwezi kuukwepa kamwe kwani ni wajibu wa kikatiba na kizalendo kwa Nchi yetu!

Naomba niwe wazi katika mjadala huu kuwa,wakati viongozi wangu wanatembea huko duniani kwa lengo la Nchi kuweza kuvutia mitaji kutoka nje,Tanzania LAZIMA ihakikishe inalinda heshima yake hasa katika mapambano dhidi ya rushwa ambayo imekuwa ikipanda kila mwaka,na hii ni kwa mujibu wa Shirika la Transparency International Corruption Index report ya mwaka 2020.

Katika andiko la karibuni kutoka KIEL Centre for Globalization lenye kichwa cha habari”Foreign Direct Investment & Corruption in Sub- Sahara Africa”(July 2019),andiko hilo linaibua mambo makubwa mawili yatokanayo na uwekezaji kutoka nje kuja barani Afrika;

1.Uwekezaji wowote kutoka nje unaweza uje na kitu kinaitwa “transmission of norms”Norms zinazoongelewa hapa ni corruption related norms za mashirika mengi ya kibepari ya uwekezaji.

Nendeni mkasome vizuri na kwa umakini andiko la ndugu yetu Javorcik (2009),Corruption & Cross Border Investment in Emerging Market.

Swala la msingi kwetu kama Nchi, lazima tuhakikishe; moja, tunavutia wawekezaji,lakini la pili,tunakagua mitaji na practice za wawekezaji hao huko walikotoka kabla ya kuja Nchini na kamwe tusivutike na uzuri na ukubwa wa miradi yao wanayotaka kuja kuwekeza hapa Nchini kwani madhara yake kisiasa kwa Taifa letu yaweza kuwa makubwa kuliko tunavyodhani!

2.Uwekezaji wa nje pia unakuja na kitu kinaitwa”increase of economic activities” yaani kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi ndani ya Nchi husika!Rejea andiko la (Sandholtz & Gray ,2003).

Kukua kwa shughuli za kiuchumi kuna waexpose “Government Officials & Politicians” kuwa katika pressure kubwa ya kutaka rushwa toka kwa wawekezaji hasa wawekezaji wale wenye tabia niliyoitaja mwanzoni yaani “corruption norms”.

Nanukuu”….multinational investors in …. industries are often accused of supporting corrupt elites in host-country (Moran,2011).

MADHARA NA SURA ZA UWEKEZAJI WA NJE AMBAZO SERIKALI LAZIMA IZIJUE VIZURI KABLA YA KUZISUJUDIA!

FDI

1.Uzoefu unaonyesha kuwa anguko la Serikali nyingi barani Afrika lilitokana na rushwa hivyo baadae wananchi kuweza kukosa imani na matendo ya baadhi ya watumishi wa Umma na baadhi ya wanasiasa!Rejea skendo ya Mh PM Mstaafu, Edward Nyoyai Lowassa na Richmond ya Dkt Harrison Mwakyembe!

Ni wazi kuwa pamoja na kwamba uwekezaji unaweza kutuletea ajira,kodi na miradi ya kijamii yaani CSR lakini bado hatupaswi kupuuza ulinzi wa mafanikio yetu hasa katika kupambana na rushwa kwa kuhakikisha kwamba mashirika yote yenye historia mbaya ya rushwa huko duniani,kamwe hayapati nafasi ya kuingia Nchini kuwekeza!Lazima tuwe watu wa kuishi kwa standards kama Taifa!

Katika siasa za ushindaji,masuala kama haya yanaweza kuwa ajenda kwa vyama vya upinzani kwa ajili ya “kuipin” CCM mwaka 2025,lazima tuwe macho mno na uwekezaji wa nje usije kuleta balaa kwa Chama chetu!

2.Madhara mengine ya uwekezaji wa Nje yapo katika kitu kinaitwa “securitization of investment”!Ongezeko lolote la shughuli za uwekezaji,lazima liende sambamba na Nchi kutoa ulinzi kwa uwekezaji huo!

Kuna hatari ya Serikali kujikita zaidi katika kuulinda uwekezaji wa nje kuliko kuwalinda watanzania hivyo kuweza kuhatarisha usalama wa Nchi.

Je,kwa kiasi gani sisi kama Nchi tumejianda kubalance matokeo ya uwekezaji dhidi ya ulinzi wa Taifa?

Ni wazi kuwa Nchi inaweza kuwekeza zaidi katika kulinda uwekezaji wa nje kwa sababu Serikali itakuwa inapata mapato yake kupitia uwekezaji huo lakini kuna hatari ya adui zetu wa ndani na maadui zetu wa nje, kutumia mwanya huo kutudhofisha!

3.Hapa napenda kunukuu kidogo tuu”….under circumstances where a State relies on external income to ensure it’s survival,..the regime may became more beholden to outside investors,donors and markets than to Citizens,..which has resulted in a “dependency Culture” anasema ndugu (Williamson,2010).

Ni wazi kuwa ni lazima sasa wanataaluma,watu wa vyombo vya ulinzi na usalama, waweze kushauri Mama kuwa hatuna ujanja zaidi ya kuanzia kujenga Uchumi wetu ndani alafu baadae ndio tutoke nje!Faida zinazotokana na uwekezaji wa nje kama ajira,kodi na miradi ya kijamii ni ndogo sana kuliko ulinzi wetu,heshima yetu na ujenzi wa Uchumi wetu wa ndani!

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Tumaini University Iringa & Saut Tabora na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %