0 0
Read Time:2 Minute, 32 Second

Mzee wa Drama

Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
November 13,2021.

Nchi ya “drama” imeshaanza tena,Nchi ambayo kila mtu anaweza kuamka toka kitandani usingizini na kuanza kusema lolote ishaanza tena!Bahati mbaya sana Nchi ya drama imewahi kuifanya CCM kuwa wakati mgumu mno hapo nyuma lakini hatujifunzi hata kidogo!

Tanzanian house of drama ndio iliwahi kuifufua CDM toka katika usingizi mzito wa kisiasa na CDM wakatumia drama za baadhi ya wanaccm kuweza kuteka majimbo mengi ya CCM mwaka 2010.

Drama za kina Andrew Chenge na vijisenti mnaziku buka,drama za Prof. Tibaijuka na vijihela vya mboga tuu”1Bilion+”,drama za kina ndugu yangu,Nizar Karamagi,Waziri wa nishati na madini.

Madhara na matokeo ya drama zile kwa watanzania si kila mtu anakumbuka?Kama wanaccm hatutajifunza kutokana na drama zile tulipokuwa tunaelekea uchaguzi mkuu wa 2010 basi hatuwezi kujifunza tena!

DRAMA TANO BORA ZAIDI KWA SASA TANZANIA.

  1. Drama ya Nape Nnauye dhidi ya mikopo ya JPM!Hii ndio drama hatari zaidi kwa uhai wa CCM kwa sasa kwani drama hii inaweza ikaigawa CCM,ikaligawa Baraza la mawaziri na hata kuwagawa Watanzania!Drama hii ni hatari zaidi na inapaswa kuchezwa kwa umakini mkubwa!

2.Drama ya Bwawa la Umeme la Nyerere,Medard Kalemani & January Makamba!Drama hii inauwezo mkubwa wa kuidhofisha Ilani ya CCM na Serikali ya CCM ya sasa japo wachezaji wa drama hii wanadhani wanamdhofisha Serikali ya awamu ya tano!

Unashangaa Waziri anawezaje kusema kulikuwepo na ucheleweshaji wa siku 400 wa makubaliano ya utekelezaji wa mkataba wa ujenzi wa mradi wa bwawa la umeme?Serikali ya awamu ya tano na awamu ya sita unazitenganishaje?!Mama watu wetu “wanademka” sana!

3.Drama ya Boss wa TPDC na upungufu wa mafuta ndani ya siku 15 zijazo kama mzigo wa mafuta hautaingia!

Wakati mhusika mkuu wa mafuta anasisisitiza kuwepo kwa uhaba wa mafuta ndani ya siku 15 zijazo kama mzigo hautoweza Kuingia Nchini,Waziri husika anakanusha taarifa ya kitaalam?kwani tukikiri kuwa tunaweza kuwa na tatizo je,kuna kesi gani?

4.Wiki Jana Mbunge wa Vunjo Charles Kimei aliuliza swali bungeni kuhusu kupungua kwa “route” za TRL kutoka Dar-Moshi -Arusha kunatokana na nini?

Naibu Waziri Uchukuzi Mwita Waitara akajibu swali la Mh Kimei kuwa suala la upungufu huo wa safari kwa “route” husika linashughulikiwa!Kesho yake Mkurugezi wa TRL ndugu yangu Masanja kadogosa akasimama na kukanusha kuwepo kwa upungufu wa “route” za safari husika!Serikali moja inakuwa na kauli zaidi ya moja”lack of coordination”.

5.Mzee wangu Generali Ulimwengu, mwanasiasa nguli nae anajaribu kuwa sehemu ya wapinga Chama chake mwenyewe kwa muda sasa mpaka watu wanajiuliza,je,anatumwa na nani au haya ni mawazo huru ya kwake?

Hatujakaa sawa Mh Spika Job Ndugai anajibu mapigo wakati tunajua wazi upande ambao ndugu yetu Jenerali Ulimwengu kwa sasa anautumikia!Je,kuna nini mbona drama zimeanza kutawala kila kona?

Je,tupo tayari kubeba gharama ya drama hizi kwa Watanzania?hivi mnasikia mijadala inayoendelea katika mitandao ya kijamii kuhusu drama hizi tano?Watanzania wanawaangalia huku wanachekaa!
Ole wetu kuna wakati tutahadhibiwa na watanzania hawa!

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %