0 0
Read Time:55 Second

Na Mwandishi wetu

WU®

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Awamu ya nane imechukua juhudi za makusudi za kuimarisha Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.

Dk. Mwinyi amesema hayo wakati alipofungua Kongamano la Uwekezaji na Maonesho ya Bidhaa za Viwanda kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, hafla iliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Airport – Zanzibar.

Alisema utendaji wa ZIPA umeimarika baada ya kuanzishwa kituo kimoja kinachotoa huduma za Uwekezaji (one stop centre), kikihusika na utoaji wa vibali vya ukaazi, ujenzi, usajili wa kampuni, masuala ya Kodi pamoja na mazingira.

Alisema hivi sasa Mwekezaji anaweza kupata kibali cha Uwekezaji ndani ya siku tatu endapo atakamilisha vyema taratibu kabla kwenda kituoni, huku akibainisha malengo ya Serikali ya Mwekezaji kukamilisha usajili huo ndani ya siku moja.

Alieleza kuwa Serikali inakamilisha zoezi la kuwa na Benki ya Ardhi, ikiwa ni hatua ya kutatua tatizo la upatikanaji wa rasilimali hiyo na kubainisha mipango ya kuwepo maeneo ya ardhi yaliotengwa kwa shughuli za uwekezaji.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %