0 0
Read Time:3 Minute, 8 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Desemba 8,2021.

Katika umri wangu wa miaka arobaini ndoto yangu ya kuiona Tanzania ya asali na maziwa katika maisha yangu inazidi kupotea kila siku!

Sababu kubwa ya kunifanya kukosa matumaini ya kuiona Tanzania ninayoiota ni kutokana kukosekana kwa Viongozi wenye kiu ya kufanya mambo yasiyo ya kawaida!

Ukitaka kuwa Taifa tajiri Lazima Taifa liwe na viongozi wenye njaa ya kufanya mambo ambayo sio ya kawaida katika uso wa Dunia hii hapo ndIo ndoto ya Taifa masikini kuwa Taifa tajiri inaweza kifikiwa!Mambo haya yamewezekana huko sehemu nyingine duniani,je, swali,kwanini tusiwe sisi?”Tiger Countries”.

SIONI mpango wowote mkakati wa kitaifa, “mzuri au mbaya”ambao unaweza kutufanya kutaka kuwa “superpower”wa Afrika mashariki tu achana na Afrika nzima,sioni kama upo mpango wa wazi wa kutufanya kuwa wakubwa duniani,kama upo mtu asimame na anitajie.

China wana mpango mkakati wenye sura mbaya usiku na wenye sura nzuri mchana unaitwa “One Belt & One Road”,India wana mpango wao wa kuitawala Dunia kibiashara ifikapo 2026 na wengine wengi huko duniani!

Haiwezekani Tanzania pamoja na kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za kikanda na Afrika bado hatujui jinsi ya kujiposition mpaka sasa katika eneo la uchumi na jinsi ya kutufanya kuwa Taifa kubwa ndani ya Afrika!

DUNIANI HUKO KUNA NINI KINAENDELEA?

Wanaotaka kuwa Taifa kubwa wana mipango ya wazi na mipango ya kificho katika kutimiza lengo lao!Mipango mikubwa ya Taifa ndio uifanya Nchi kuheshimika kwa watu wake na hasa wapiga kura wake!

Nchi ya Misri wana ndoto ya kuwa Taifa kubwa kupitia mpango wao na mfuko wao wa Sovereign Fund of Egpty,Iran wana National Development Fund of Iran,Russia wana Russian Sovereign Direct Investment Fund,Libya wana Libya Investment Authority,China investment Corporation,Australia Government Investment Fund na kadhalika!

Mifuko hii ya serikali ukusanya fedha kutoka vyanzo na sehemu mbalimbali kwa lengo ya kuiwezesha serikali moja(I)kuwekeza katika sekta zinazokuwa haraka na kuleta faida kubwa kwa haraka,pili(ii)kuiwezesha serikali kulinda maslahi yake katika miradi yake ya kimkakati ya kitaifa kwa maslahi mapana ya Taifa Mfano hapa kwetu ungeweza kuzungumzia mradi inaokuja wa gesi asilia ambao tunataka kumwachia wadachi wawekeze pekee yao bila sisi kushiriki.

Tatu(III)ushiriki wa serikali katika miradi hii unaweza kuifanya kupata mapato zaidi kutokana na uwekezaji huo hivyo kutanua wigo wa mapato na kushiriki katika uchumi wake yenyewe!Bahati mbaya sana mnadanganywa na wachumi wenu wa “bongo”kwamba ni mwiko serikali kushiriki katika baiashara,nani kasema?dunia ya sasa bila ushiriki wa serikali katika biashara ni kujitengenezea umasikini katika Taifa!

FEDHA ZA MFUKO HUU TUNGEZITOA WAPI?

Tanzania Investment Corporation ndio njia pekee ya kutufanya kuwa superpower angalau kwa afrika na hatuna sababu ya kusita kuanzisha mfuko huu sasa kwa sababu ya kukosa mtaji!

Kama tunataka kuwa Nchi kubwa lazima tuwe na mawazo na ndoto kubwa kuanzia ndani ya Ilani ya CCM mpaka kwenye mipango yetu ya kitaifa na “road map” hiyo lazima iweze kubebwa na kiongozi yoyote tutakayemchagua lazima ajue kwamba anaenda “kuidrive” ajenda hii ya Taifa!

Fedha ya mfuko huu tungeweza kuipata (I)Magawio kutoka mashirika ya Umma(Ii)migodi yetu(III)bajeti kuu ya serikali(IV)mikopo ya kibiashara toka IMF na WB.

Hivi leo hii kweli tungeshindwa kufinance mradi wa Bandari ya Bagamoyo au mradi wa gesi ya kusini angalau kwa kuingiza mtaji nusu tu ya uwekezaji mzima wa miradi husika!

Tukiendelea kuwaza kimasikini masikini itatuchukua miaka hata elfu moja kuwa Taifa kubwa Afrika!Naogopa kuwa sehemu ya kizazi kinachowaza mambo rahisi rahisi tu kila siku.

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Saut & Tumaini Iringa na mtia Nia ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %