

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
January 1,2022.
Ni siku mpya ya mwaka mpya, sifa na utukufu zimrudie Mungu Baba yetu wa mbinguni atupaye pumzi ya kuweza kuishi hapa duniani, mpaka leo tukaja kuuona mwaka mpya mwingine tena wa 2022.
Kwa mara nyingine tena,Mungu ameweza kuniongoza kuwaambia wale wote ambayo Mungu amewapa nafasi ya kipekee kufanya kazi kwa karibu na Mh.RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan.
Nianze kwa kusema kuwa, taasisi hii ya urais na Mh.RAIS mwenyewe, sio tu kwamba wanapaswa kulindwa kwa silaha za moto pekee dhidi ya maadui wa Taifa, lakini pia Mh RAIS anapaswa kupewa ulinzi wa kiakili,kiroho na hata kiafya ili aweze kutekeleza na kutimiza majukumu yake ya kikatiba na majukumu yake ya kiraia ya kuwaongoza watanzania hawa weweze kufikia malengo yao kama Taifa!
Mfano, Mheshimiwa Rais akikosa utulivu wa kiakili yaani “mental stress”lazima atashindwa pia kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa kiwango cha juu, hivyo anaweza kushindwa kufikia malengo yake binafsi,malengo ya chama chake na hata malengo ya kitaifa!
Gharama,akili na uzito tunayotumia kumlinda Mh Rais dhidi ya “physical harm”, unapaswa kuwa sawa sawa na nguvu tunayotumia kumlinda”protect” dhidi magonjwa,misongo ya mawazo na mambo mengineyo ambayo mengine sitoweza kuyataja hapa!
Ndio maana wakati mwingine,kazi hizi nyeti kama za Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,zinahitaji mtu ambaye ni zaidi kujua uandishi wa habari ambaye labda anafahamu nini maana ya kuilinda na kuikuza brandi nzima ya urais na kuweza kukubalika mbele za watu wote!Rais ni kama bidhaa na mwisho wa siku iwe mbaya iwe nzuri, lazima iweze kuuzika sokoni!Period!
Bahati mbaya sana tunadhani kwamba, mwandishi yoyote wa taaluma ya habari, anaweza kuifanya kazi hii bila kupwaya na hapo ndipo tunapokosea!
TANGIA kuzuke mjadala wa Serikali kukopa kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo na hatimaye Mh Rais kupata upinzani wa wazi kutoka mhimili mwingine za dola,Si Msemaji wa Serikali wala si Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ameweza kusimama na kujibu hoja kwa lengo la kumlinda Mh.Rais wetu asichafuliwe dhidi ya shutuma hizo!
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali, wanapaswa kuwa “cover” ya Mh. Rais kabla hajafikiwa na Mtu au kitu chochote kile!
Wakati mwingine unaweza “ukanote” udhaifu wa Serikali haraka kutokana tu na kukosekana kwa watu wenye weledi wa kulinda taasisi ya urais na RAIS mwenyewe LAKINI pia;unaweza “ukanote” uimara wa Serikali na taasisi ya urais, kutokana na kuwepo watu wenye weledi na makini wanajua jinsi ya kuitengeneza na kuilinda taasisi ya urais kupitia mawasiliano mkakati!
Moja wa awamu ambayo inatajwa kuwa na kurugenzi bora ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ni wakati wa Rais wa awamu ya tatu na awamu ya nne wa Tanzania!Nchini Kenya,Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu anayetajwa kuwa kinara wa kumlinda Rais Mwai Kibaki alikuwa anaitwa Bwana Mutua!Hivi ndivyo inapaswa kuwa.
Haiwezekani “brand” au taasisi ya urais inashambuliwa mchana kweupe, watetezi wake Mh Rais wakawa wapo kwenye usingizi mzito, wakiwaacha watoa “nongwa” wakitamba usiku mchana katika majukwaa yao mbalimbali ya habari, huku wenyeviti wa CCM Mikoa ndio wakibeba jukumu la kumpambania na kumlinda “Kamanda” wao huku watu wenye taaluma zao wapo kimya KABISA maofisini!
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu lazima awe na akili kubwa kuweza (I)kusoma kwa haraka sana lengo la ndani mtoa hoja”hidden ajenda of a source”(Ii)kusoma kwa haraka public upinions inasomaje kuhusu hoja husika(iii)na kuweza “kuconsolidate” taarifa ya haraka ya
kujibu hoja husika kwa nidhamu,usahihi na takwimu za wazi kuhusu hoja husika!
Uwezo huu wa kuweza kuzicontain (I)hoja ya mtoa hoja(Ii)na public opinions kwa pamoja ndio uzaliwa watu wanaitwa “spin doctors” kwenye mawasiliano ya kitaasisi!Hawa ni watu maalum wenye taaluma zaidi ya moja ambao Chakula chao chao cha kila siku ni taarifa taarifa taarifa!
Kusa popote unapotaka kugusa kuhusu taasisi ya urais,watu hawa watakujibu kwa usahihi na utulivu mkubwa, huku wanatabasamu na mhusika anaishia kukubaliana nao hivyo kuifanya taasisi ya urais na RAIS kuweza kung’ara kila siku!
Kwa Nchi kama Marekani watu hawa “press secretary” uandaliwa kwa muda mrefu kuja kuchukua majukumu haya!Umeona na unamkumbuka Msemaji Mkuu wa Serikali ya Iraq wakati wamerkani wanaingia Bagidad?
Uwezo wa kumlinda Rais wako dhidi ya propaganda mpaka siku ya mwisho ndio sifa kubwa ya spin doctors!
Mwaka huu wa 2022 uwe mwanzo mpya wa kuweka sawa mambo yetu pale Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu!
Mh hakupaswa kumjibu yule jamaa wa Dodoma kwamba”TUTAKOPA”,yule alikuwa ni saizi yako Jaffary Haniu au Gerson Msingwa,you need to be coordinated as one team!

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Chuo Kikuu Saut & Tumaini Iringa na Mtia Nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.
+255784159968.
MWAKA 2022 NA KAZI IENDELEE!
Hakika nimefurahishwa na “Comment” zako George Michael Uledi. Naamini wahusika wataifanyia kazi. Uandishi hatukuuanzisha sisi wabongo. Wabongo tumejifunza toka kwa wazoefu wa uandishi toka Ulaya na Marekani. Nasikitika kusema wengi wetu tumejifunza kunakili. Nakumbuka tulikuwa na somo pale Radio Netherlands Training Center kule Netherlands walilotufundisha kuwa “Media is Power”. Humo tulifundishwa namna Media inavyoweza kubadilisha mwelekeo wa fikra za watu kuhusu utawala uliopo au unaotarajiwa kuja. Matumizi ya Media kwa namna hiyo tunayaona kila siku katika Media za Wazungu na Wamarekani. Kila kukicha habari za kipaumbele kuhusu Afrika ni vita, njaa, mauaji, umasikini, udhalilishaji. Ukisikia, kuona, kusoma habari hizi kila kukicha, mwisho wa siku tunaaminishwa kuwa Afrika ni bara la njaa, umasikini, ukandamizaji, mauaji, vita na kadhalika. Cha ajabu hata sisi wenyewe waandishi wa Afrika tuna “copy & paste” habari zinazotudhalilisha wenyewe na kuziweka vichwa vya habari kwa wino ukiokolezwa! Imefika mahali waafrika tunaamini Wazungu wala Wamarekani, hakuna anayelala njaa, hakuna masikini, hakuna wagonjwa. Yaani Ukata na Marekani ni raha tupu siku 7 za wiki, miezi 12 ya mwaka. (Kama mimi mwongo, ajitokeze mwandishi afanye utafiti kuuliza wabongo iwapo wanajua kuwa kuna wazungu wanalala na njaa, hawana makazi, wanakula mlo mmoja kwa siku)…. Nikirudi kwenye mada ni kuwa, anachosema George ni kweli kabisa. Tuliyojifunza majuu (Nchi za Magharibi) tuyafanyie kazi. Msemaji Mkuu wa Serikali anaisemea Serikali na Rais wake. Mwandishi wa Rais anamsemea Rais. Lakini wao pia ni washauri wa karibu wa Rais. Iweje leo Rais anaacha shughuli zake za kuendesha nchi na kuingia kwenye majibizano? Halafu anayejibizana naye kesha kula matapishi yake mwenyewe? Dennis Moyo, former Senior Editor Swahili Redacteur, Voice of Germany Deutsche Welle.
Denis asante kwa comment zako nzuri, karibu sana WABONGO UGHAIBUNI WU, UKIJISIKIA KUANDIKA KUCHANGIA MAWAZO NA USHAURI KWA MAENDELEO YA NCHI YETU CONTACT US- info@tzabroad.com