0 0
Read Time:2 Minute, 10 Second

Na Dr Yahya Msangi

Togo

West Africa

Miaka ya 1930-40 wajerumani wengi walitenda ouvu wa kutisha dhidi ya binadamu wa mataifa mbalimbali chini ya falsafa ya NAZI. Muasisi Hitler alipoona mambo yanaharibika alijipa hukumu mwenyewe na mkewe. Wenzie waliamua kujificha.

Baadhi ilipita miaka hadi 50 wakidunda. Wengi waliamini wame save ngoma. Wengi waliamua kukimbilia America ya kusini haswaa nchini Argentina. Wakafungua biashara na kuendelea na maisha raha mustarehe. Lakini baadhi ya watu waliamua kuanzisha kampeni iliyoitwa HUNT DOWN THE NAZI. Kampeni hii ilihusisha taasisi kama MOSSAD (shirika la ujasusi la Izrael), vyombo maarufu vya Habari kama ABC na familia za wahanga. Hawakujali sheria iliyopitishwa na serikali ya German kusitisha zoezi la kuwasaka MANAZI.

Binafsi naona jambo moja Tanzania ambalo Mtu anaweza kuja kuwajibika baadaye. Jambo lenyewe liko wazi mno. Ushahidi upo wazi mno. Hauna Shaka. Si wa kuhisi!

Jambo lenyewe ni: wabunge 19 (C19 girls). Kitendo hiki ni uvunjifu wa wazi wa KATIBA na sheria ya VYAMA. Wahusika wakuu ni Spika na C19 girls. Hâta wangetoa ufafanuzi kutwa bado haifuti ukweli Kuwa katiba imesiginwa na Sheria imevunjwa waziwazi.

BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Iko siku ama kikundi cha watu au Mtu atazmua kuiomba mahakama iwaadhibu wahusika. Unaweza isiwe Léo wala kesho lakini ipo siku! Mjiandae kulipa na fidia.

Uhalifu huu hauwezi ukaulinganisha na madai sijui ya watu kutekwa, kupoteza au kupigwa fimbo au risasi! Au viroba kuonekana baharini!

Uhalifu huu uko na ushahidi unaojitosholeza.

Na bahati mbaya ni kwamba wengine pia wanaweza kuja kuhusishwa na kesi hii. Wale au yule aliyeapa kuilinda katiba! Wale woote ambao walitambua au kuhalalisha ubunge huu wa C 19 Girls! Inashangaza wapinzani na chadema yenyewe haijaona umuhimu wa kufungua shauri kuhusu jinai hii iliyo wazi! Ingelipa kuliko vikesi uchwara.

Ili kuepuka haya ni vyema wale ambao wamebariki uhalifu huu overtly or covertly wachukue hatua sasa! Bunge sio mali ya “nimekosea sasa, nimekosea sana”! Bunge ni mali ya watanzania. It’s very simple kurekebisha. Hâta hii kudai nchi itauzwa ni kiburi kinachotokana na watu kuacha mtu afanye bunge ni mali yake! Afanye atakavyo! Atashindwaje kudai nchi itauzwa wakati alipoteua wabunge wake hamkumkemea?

Hâta C19 girls ingekuwa wanaona mbali wao wenyewe wangejiuzulu.

Lakini kama ilivyokuwa kwa wale MANAZI watu wanaweza kuziba masikio na kujidanganya hawataguswa kamwe.

Mbunge Halina Mdee

Until when it happens!

Nirudie : UWEPO WA C19 GIRLS BUNGENI NI UHALIFU UTAKAO WAATHIRI WAHUSIKA BAADAYE

TYL: “NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO” Sipendi mtu napenda nchi.

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kawe Mwanachama wa Chadema na kwa Sasa ni Mbunge wa Viti maalumu, Halima Mdee baada ya Msiba aliamua kuibusu picha ya Hayati John Magufuli kama ishara ya maombolezo.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %