0 0
Read Time:1 Minute, 15 Second

George Michael Uledi!
Kyela,Mbeya.
January 4,2021.

Acha waendelee kutengeneza maneno na majungu lakini ni kama serikali ya awamu ya sita, imeamua kukaa kimya na kusema wacha wayaone wenyewe, pale Mh RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan,leo mchana wa SAA Nane, atakapokuwa anapokea taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kupitia mkopo toka Banki ya Dunia wa shilingi Tsh Trilioni 1.3!

Juzi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa,jana amewapongeza wakuu wa mikoa na wilaya Tanzania nzima, kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa miradi hiyo ambayo inaenda kugusa kila mtoto wa mtanzania masikini Nchi nzima!

Huku wapinzani wa Mama Samia Suluhu Hassan, wakiangaika usiku na mchana kutaka kukwamisha nia njema ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia,sisi tumeamua kuwajibu kwa matendo na matokeo ya kazi nzuri za Serikali ya CCM ya awamu ya sita!

Wale wote wanaoeneza uzushi kuhusu afya ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan ,utadhani kuumwa binadamu katika Nchi hii ni kosa la jinai, watasubili sana!

Watu hawa na mitandao ya namna hiyo, ambayo ina nia na inalenga kuleta taharuki ndani ya Taifa twapaswa kuipuuza,(TanzaniaLeaks) na wenzao!

“……Uhuru wa habari wako unakomea pale unapoanzia uhuru wa mtu mwingine…”.

Mwandishi ni kada wa CCM,Ofisa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli, Arusha,Mhadhiri wa zamani,vyuo vya Saut & Tumaini Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %