0 0
Read Time:4 Minute, 44 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya!
January 5,2022.

Desemba 31,2021 siku ya mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya, niliweka hadharani makala yenye kichwa “mpango kificho” wa adui dhidi ya Mh. Rais Mama Samia Suluhu Hassan na kuandika”MAMA SAMIA HII NI VITA”.

Leo Mh.Rais, Mama amekiri kuwa hii ni vita ya kuutafuta urais ndani ya CCM kuelekea mwaka wa uchaguzi wa 2025 na hapa ninanukuu!

“…Hauwezi kufikiria kwamba mtu unayemuamini,kiongozi wa mhimili, aende akaseme yale,ni stress za 2025…”.

“….kwa wale ambao ndoto zao ni 2025 nitawaweka kando ili wapate muda zaidi wa kujiandaa ili tukutane huko 2025…”.

Kwa kauli hizi mbili kati ya nyingi ambao Mama Samia Suluhu Hassan amezitoa jana, ni wazi kwamba, sasa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Samia Suluhu Hassan,sasa kashaamua kuingiza majeshi yake katika uwanja wa medani rasmi!

Baada ya uvumilivu wa muda dhidi ya waroho na wasaka Ikulu kabla ya kipenga,Mh Rais kaamua kufungua kuwaonyesha watu hao ndani ya CCM kwamba na yeye yupo na yupo imara kabisa!Nanukuu;

“…..wakati mnanikabidhi huu mzigo(2021),nilianza kusikia lugha za Serikali ya mpito bungeni huko kwa kina kasim………”

Hakuna “options” nyingine zaidi ya hizi mbili kwa Mh. Rais wangu kwa sasa(I) akubaliane na wataka urais ndani ya CCM kwamba mwaka 2025 hatogombea na hii itachochea sana “faulo” za kisiasa kuanzia sasa hivyo malengo ya Serikali yake na malengo ya Ilani ya uchaguzi ya CCM 2020/25 yanaweza yasitimie(ii)au amue kupambana nao maadui kama Mwenyekiti wa chama Taifa kwa lengo la kuendeleza umoja na mshkamano kuelekea mwaka 2025 ndani ya chama chake!

MPANGO VITA WA MH.MAMA SAMIA SULUHU HASSAN MPAKA DAKIKA HII UMEKUWA BORA SANA!

Ushindi dhidi ya adui vitani ama kwenye uwanja wa medani upatikana kwa kuainisha matumizi sahihi ya kitu kinaitwa”Principles of War”!Matumizi sahihi ya kanuni vita ndio mpaka sasa yanamfanya Mh Rais aonekane ameutawala uwanja wa medani mpaka sasa dhidi ya kauli zenye utata kutoka mhimili wa Bunge!

1.Mh Rais Samia Hassan kwanza ameweza kutumia kanuni sahihi katika vita hii kwa kuweza kutumia kanuni namba moja ya vita yaani”Selection & maintainance of the Aim”!

Ni wazi kuwa kitendo cha Mh.Rais Samia Suluhu Hassan, mpaka sasa kuweza kusimama na kauli yake kuhusu kukopa fedha nje ya Nchi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo, inaendelea kumpa heshima na uhalali wa kisiasa dhidi ya wapinzani wake!Achana na mjadala wa tukope au tusikope,lakini kusimamia anachoamini ndio kuaminika kwake!

….TUTAKOPA….”
“Siwezi nikawadanganya hapa kwamba sitokopa,TUTAKOPA……”.

Hii ndio kanuni ya kwanza ya vita yaani kamanda kuweza kutotoka kwenye lengo lake kuu la kivita!

Kusimamia lengo lako kuu uliloamua kulichagua na kulifanyia kazi katika uwanja wa medani kama Kamanda ndio roho ya ushindi vitani katika kutekeleza mpango vita!Kanuni vita hii pia inaweza/imeweza kutumiwa na wanasiasa na kuweza kupata matokeo ya kisiasa!

2.Kanuni ya pili ya vita ambayo Mh Rais Samia Suluhu Hassan kaitumia katika kumkabili adui inaitwa “Surprise the Enemy”.Hakuna aliyetarajia kuwa hotuba ya Mh.Rais leo ingekuwa na majibu ya wale wote waliothubutu kupinga hadharani mipango yake ya kukopa nje!

Kitendo cha Mh. Spika Job Ndugai kuomba msamaha hadharani jana, inawezekana kimetafsiriwa kuwa ni unafiki tu na hakina nia njema na ni kitendo cha kimkakati wa kiwango cha juu hasa kwa mtu anayesimamia mhimili “critical” kama Bunge linaloongozwa na CCM kwa viti zaidi ya asilimia 95+.

Kwa vyovyote, majibu na ufafanuzi wa Mh Rais leo hii, hakutarajiwa sio tu na Mh. Spika Job Ndugai, lakini pia haukutarajiwa na watu wengi lakini kwangu mimi, ufafanuzi ule ulikuwa hauepukiki kwa sasa, na ilikuwa lazima kwa Mh. Mama Samia Suluhu Hassan aseme kumwonyesha adui kuwa anaijua kwa undani mipango yao ya kusaka Urais 2025!Hii ndio njia sahihi na rahisi ya kumshambulia na “kumcontain” adui yake,always make sure you surprise your enemy!

3.Kanuni nyingine ambayo kaitumia Mh. Mama Samia , katika kuwakabili adui zake leo, katika hotuba yake inaitwa matumizi ya kanuni ya “Offensive action”!Sioni dalili wala sitarajii kuona kwamba “adui” zake wanaweza kujibu mapigo haya mazito ya Mh Rais !Sioni!

Unashauriwa ukiamua kuvamia ngome ya adui yako basi hakikisha unaipiga ngome yake kisawasawa kwa akili na nguvu zako zote!Nanukuu;

“…hivi karibuni ntabadili Baraza la mawaziri,….wale ambao ndoto zao ni 2025 nitawaweka pembeni,ili wapate muda wa zaidi wa kujiandaa ili tukutane huko 2025…”!

Ni wazi kuwa Mh. Rais alishafanya kazi ya kutosha ya kupembua maadui/wafuasi wake tangia kitambo, kwani mkeka mpya unaenda kugusa mpaka mawaziri!Hii ndio maana halisi ya “offensive action” kwa adui zako!

USHAURI WA BURE KWA MAMA SAMIA!

Kamwe asikubali kurudi nyuma katika mpango huu, kwani ishara yoyote ya kuweza kurudi nyuma itamfanya adui zake wadhani yeye ni muoga dhidi yao!

Adui wa Serikali ya CCM wapo wengi japo wapo kimya, kwahiyo kazi ya kuwatambua na kuwachomoa lazima iendeleee!Bora uondoke na kundi dogo la askari kwenda vitani kuliko kubeba kundi kubwa la askari waasi,hauwezi kushinda vita dhidi ya umasikini na maendeleo ya Taifa!

Mawaziri sawa lakini bado kuna makundi mengine mengi ndani ya maRC,DC,DED,Wabunge na CCM na kwingineko ndani ya Serikali ambao pia ni kikwazo kwa utekelezaji wa ilani ya CCM na malengo ya Serikali ya CCM ya awamu ya sita!

Muda wa karibia mwaka mmoja uliokaa madarakani nadhani umetosha kuwajua wafuasi wako,mawaziri wachapakazi wako,makada wa CCM watiifu kwako na mengine mengi!

Fanya maamuzi sahihi bila kuonea mtu!kazi iendelee!

Mwandishi ni kada wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi vyuo Vikuu vya Saut & Tumaini Iringa na Mtia Nia Ubunge CCM Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %