0 0
Read Time:45 Second

Na Mwandishi wetu WU ®

Zanzibar

Tanzania Diaspora Hub wapo katika Ziara ndefu ya kuzunguka Tanzania kwa Nia ya kufuatilia fursa za uwekezaji Pamoja na kufanya mikataba ya kibiashara,sasa wapo Zanzibar, Leo wakiwa Micheweni Pemba wametembelea kituo Cha Watoto yatima na kutoa sadaka. Katika msafara huo ambao umeongozwa na wawakilishi wa IDARA unayo shughulika na Diaspora Zanzibar, Ndugu Mahfoudh Othman Soud na Ndugu Ali Ameir Haji wakiwa na uongozi wa TDH waliopo kwenye ziara hiyo ya kikazi , Nassoroh Ally Basalama, Proffessor Leonard Munghor, Norman Jasson na Emil Mutta Agustino, walikabidhi sadaka hizo kwa sheikh Khamis wa Nyumba ya watu Wema Micheweni. TDH ni umoja wa Watanzania ughaibuni, Pamoja na uwekezaji lakini pia wanatambua kuwa lazima waangalie mahitaji ya jamii inayozunguka katika maeneo ya uwekezaji wao alisisitiza Hilo Mkurugenzi wa TDH Nassor Ally Basalama alipokuwa akiongea kwa niaba ya TDH Duniani wakati wa kukabidhi Sadaka hizo.

TDH WAKIKABIDHI SADAKA
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %