
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya!
January 5,2022.
Mh.Spika Job Austin Ndugai wanaokudanganya kuwa wewe ni mhimili huru dhidi ya dola hawana nia njema na wewe na hawataki uilinde heshima yako ya baadae ndani ya CCM na utumishi wako!

Kumbuka mhimili wako unajengwa na asilimia zaidi ya 95+ ya wabunge wa CCM lakini pia hata wewe mwenyewe Mheshimiwa Spika, Uspika wako unatokana na chama chako cha Mapinduzi!Na kama Uspika wako unatokana na chama chako cha mapinduzi, kwahiyo ni uongo “in practice” kusema wewe ni mhimili huru dhidi ya dola ya Serikali yako ya CCM!
Hauwezi kuwa na wabunge asilimia zaidi ya 95+ wa CCM chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa,Samia Suluhu Hassan alafu wakakuacha salama kwenye kikao kijacho,infact vita hii wanaenda “kuinunua”wabunge wako mwenyewe Bungeni kwenye possibly kuanzia kikao kijacho kama ambavyo waliinunua wenyeviti wa CCM Mikoani na ndani ya matawi mengine ya CCM!
Mh.Spika naiona kesho yako itakuwa ngumu mno!Mzee wangu Spika Job Ndugai usitegemee Mwenyekiti wa CCM “atadeal” na wewe kisiasa kwa sasa, lakini nina uhakika matawi yake ndio “yatadeal” na wewe na ili uweze kulinda heshima yako ndani ya CCM na Bunge lako, nashauri waachie Bunge lao,kapumzike!
Mhimili wa dola najua unajua kuwa una taarifa zako za kila aina so far na utaendelea kuwa na taarifa zako always!Njia bora ya wewe Mh.Spika kujitenga na kundi la wasaka Urais ndani ya CCM kwa sasa, ni wewe kwenda Nyumbani Kongwa kupumzika tu!Mhimili wa dola hauwezi kuja na taarifa za “kukuaccuse” mtu wa nafasi yako bila kuwa na uhakika na taarifa hizo!Hapa hamkuplan vizuri na wenzako,it was too early kuja na mpango huu for now!
Kwa kifupi, tunaambiwa kuwa na mhimili dola kuwa siku ile wewe haukuwa unaongea kama “Mhimili” wa kutaka kuishauri Serikali bali ulikuwa unaongea kama sehemu ya kundi la wasaka Urais 2025.
Sasa kwanini watu wa pembeni yako leo hii wanaangaika tena wanataka kutuaminisha kuwa wewe ulikuwa unaongea kama “Mhimili huru”, wakati sio kweli?Naona kuna dalili za wazi za siku si nyingi za kuanza kushambuliwa na wabunge wa CCM katika kikao kijacho cha Bunge!
Mh.Rais Ally Hassan Mwinyi,Rais wa awamu ya pili, aliweza kujiuzuru nafasi yake ya Uwaziri wa Mambo ya ndani miaka fulani na kitendo HICHO kumpa heshima kubwa mbele ya safari kwa makosa ambayo hata hakuyafanya yeye!Alikuwa anatafuta heshima tu ndani ya CCM na ndani ya Serikali yake!Inatokeaga!
Edward Ngoyai Lowassa ,Waziri Mkuu mstaafu, aliweza kujiuzuru kwa kushutumiwa na kamati ya Bunge na Bunge likamwondoa!
MH.SPIKA JIUZURU KUEPUKA HAYA YAJAYO!
1.Kikao cha Bunge lijalo lazima kitaanza “kudeal”na wewe na usipokuwa makini kuna vurugu kubwa zaweza kutokea,njia bora hapa ni kupisha tu, afterlow umebakiza miaka michache tu KWANI ulishasema hautorudi tena Jimbo,Kongwa.
2.Matamko yanayoendelea kwa sasa kutolewa na jumuiya za CCM hayana ishara nzuri kwako na matamko HAYA ni wazi yana baraka za Chama!Ni suala la kupima tu kipi bora kati ya CCM na uspika wako wewe kama Job Ndugai!Pima mapema Mkuu wangu!
3.Kwa bahati mbaya,Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio huyo huyo Mwenyekiti wako wa CCM na ndio huyo huyo anasema una homa ya 2025!Rais huyu ndio anayesimamia mchakato mzima wa uteuzi wa wagombea ubunge mwaka 2025 na chaguzi zijacho mwaka 2022 ndani ya CCM!Unadhani kuna Mbunge wa ccm mpaka hapo anaweza kusimama na wewe for now???Pima ushauri WANGU Mh.Spika!
4.Uamuzi wako ambao utakuwa sio sahihi na mbaya ni wewe kuamia(I) upinzani kuendeleza mapambano hivyo utakuwa umethibitisha kuwa kweli ilikuwa homa tu ya mwaka 2025!
Uamuzi wako kutaka kuendelea kubaki na Uspika na wasioona mbali wanadhani eti unaweza “kumpigisha kwata” Mh Rais la kutokuwa na imani nae”vote of no confidence”!Hiyo nguvu hauna kwa sasa na wala USIJARIBU kwani itaendelea kukushushia “P” zaidi!Ushauri wangu Ondoka hata kesho!Utakuwa umejenga heshima kubwa ndani ya CCM na heshima ya kwako wewe mwenyewe!
5.Wanasema if you can’t beat them join them.Kwa upepo huu, nakushauri ungana nao ili kuweza kufuta ile kauli ya homa ya mwaka 2025, otherwise ile kauli haitofutika kwa wewe kuendelea kukalia kiti!utakufa nayo,kauli kitanzini!
HAYA matamko yanayotoka ndani ya CCM ni ishara mbaya kwako kwa sasa!Cut the story short, waachie uspika wao,nongwa itakuwa imekwisha!
Nakushauri usiwarudie kuomba ushauri kwa wale walikutuma kama wapo kwani ndio watakuwa wanakuharibia zaidi Mzee wangu Job Ndugai!Hii ni ajali ya kisiasa na wewe hautokuwa mtu wa kwanza kuinasa!
Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi Vyuo Vikuu vya Saut & Tumaini Iringa,Mtia Nia Ubunge CCM Jimbo la Kyela 2020.
+255784159968.








