0 0
Read Time:33 Second

Na Mwandishi wetu WU®

AKADEMI ya AS ROMA, imetajwa kuwa na mchezaji mwenye asili ya Tanzania, Giulio Lachini ambaye ni mmoja Kati ya Watoto wa Diaspora wa Kitanzania Ughaibuni.

Kwa mujibu wa Paul Johnson, Diaspora anaeishi Italy amesema mama yake Giulio ni Mtanzania.

Mpaka sasa Tanzania bado haijapitisga sheria ya uraia pacha hivyo Giulio kuchezea Taifa Stars hata kama mama yake ataweza kumshawishi lakini sheria hairuhusu.

Tanzania ilipoteza fursa ya kumpata mshambuliaji wa RB Leipzig inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani, Yussuf Poulsen, ambaye angeweza kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania sababu baba yake ni Mtanzania mwenye asili ya mkoa wa Tanga, lakini akachagua kuchezea timu ya taifa la mama yake, Denmark.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %