

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Desemba 7,2022.
Ni upotoshaji mkubwa kusema Mh Job Yustino NDUGAI ameshurutishwa kujiuzuru nafasi yake ya Uspika wa Bunge na dola au chama chake!Sio dola wala chama chake, CCM ambacho kiliwahi kumshurutisha siku yoyote na mahali popote nje au ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Wapinzani wa CCM wameamua sasa kutaka kutumia kujiuzuru kwa Mh. Ndugai kwa kutaka kutumia tukio hilo kama mtaji wao wa kisiasa kwao kwa manufaa ya kisiasa!Mh Job Job Ndugai hakuwahi kupata shinikizo “rasmi” lolote kutoka chama cha mapinduzi na mahali popote!
Kelele za kumshauri Mh. Job Yustino Ndugai ziliweza kutoka ktk makundi mbalimbali ya kisiasa na kijamii kwa maana ya wanasiasa wa upinzani,wanaharakati wa haki za wanawake,washika dau wa elimu na maendeleo na makundi mengine!
Vijana wa wale wa CCM kama yalivyo makundi mengine ya kisiasa na kijamii yalikuwa yanatumia haki yao ya kikatiba kumshauri na kumtaka Mh. Job Ndugai ajitathimini na kufanya uamuzi kwa heshima yake mwenyewe!
NI UTARATIBU WA CCM MARA ZOTE KUTUMIA VIKAO KUWAJIBISHANA!
1.CCM kama chama dola na chama cha mfano barani Afrika,hakijawahi na wala hakitowahi kutumia “Press Conference” kama njia ya kufikia maamuzi ya chama zaidi ya kutumia VIKAO halali ndani ya chama!Ni kukikosea heshima chama chetu cha Mapinduzi kwamba kilitumia njia yoyote ile kumsurutisha Ndugu na Mh.Job Ndugai kujiuzuru, kama wasemavyo wapinzani wetu!
Kwa maana hiyo,hakuna kikao kilichoitishwa na CCM, siku yoyote wala mahali popote kupitia kwa Katibu Mkuu wake Daniel Chongolo, wala kwa Msemaji wake Ndugu Shaka Shaka na kuzungumzia kuhusu kujiuzuru kwa Mh. Job Austino Ndugai!Maamuzi ya Mh.Job Ndugai ni maamuzi yake binafsi ambayo hayafungamani na shinikizo kutoka CCM kwa vyovyote!
2.Pili,hakukuwa na kikao chochote na mahala popote cha Serikali”Dola” kilichokaa kwa nia na madhumuni ya kumshurutisha Mh Job Ndugai ajiuzuru!Hakuna!
Ufafanuzi wa Mh. Rais Samia Hassan Jana, haukuwahi kumshauri wala kumtaka Mh Job Yustino Ndugai ajiuzuru zaidi ya kujibu hoja zake katika MAUDHUI ya kisiasa kuhusu umuhimu wa Nchi kukopa kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania!Dola ya CCM haina nia wala mamlaka na wala muda wa kuingilia Mhimili mwingine hivyo itaendelea na ingeendelea kuheshimu maamuzi yoyote ya Mh Job Austino Ndugai yakiwemo kuendelea na Uspika wake mpaka mwaka 2025 au laa!
3.Mh Job Yustino Ndugai kama kiongozi mahiri wa CCM ,alijipima mwenyewe kwa kuzingatia tamaduni,ustaarabu na heshima ya CCM kisha kuamua kwa hiari yake kufanya maamuzi aliyofikia!Sio mara ya kwanza kwa makada wakuu wa CCM kuweza kufikia maamuzi kama haya ya leo na huu ndio utamaduni wa CCM miaka nenda rudi!
Waziri Mkuu wa wakati huo Edward Lowassa aliamua kujima na kuamua kuwajibika bila kushurutishwa na CCM kwa wakati ule!Mh Rais Ally Hassan Mwinyi, aliwahi kujipima na kuamua kujiuzuru miaka fulani kabla hajawa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miaka ya 1980!
Ni wazi kuwa,Mh. Job Yustino Ndugai sasa anafungua fursa mpya kwake mbele kwa nafasi zingine ndani na nje ya Serikali ambazo ataonekana anafaa na kuweza kuwatumikia watanzania na chama chake pia!
Serikali ya awamu ya sita ya Mh Mama yetu Samia Suluhu Hassan itaendelea kuheshimu Mihimili mingine ili kila mhimili uweze kufanya majukumu yake kwa maslahi ya Taifa!CCM imekuwa imara zaidi kuliko Jana!
Mwandishi ni Kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Vyuo Vikuu vya Saut & Tumaini Iringa na Mtia nia Ubunge wa CCM Jimbo la Kyela 2020.
+255784159968.








