0 0
Read Time:3 Minute, 38 Second

Na Cde. Happiness Mgongo
Chamwino_Dodoma MNEC_VITI15 BARA

Mapinduziii
Daima Tutayalinda na ni mkombozi wetuuu.

Abeid Karume in 1964

Kila tarehe 12.01. huwa ni Kumbukizi ya Maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambapo Huwa yanakumbusha namna ambavyo Wazanzibari walivyoweza kujikomboa kutoka katika Minyororo ya kisultani ambayo iliwanyina uhuru kwa kila kitu yaan; kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na hata kijamii.
Kwani wazanzibari walidharauliwa,wakifanywa watumwa, walicharazwa bakora na kuambiwa walipe kodi kwa mabwanyenye hao wa kisultani huku uchumi wa Zanzibar ulinufaisha Nchi za kiarabu na kingereza ambao walikuwa wakiingia Zanzibar na kujinufaisha kupitia watumwa, pembe za ndovu na madini mbalimbali,

Tangu mwaka 1840 ambapo sultan seyyid said alipoamua kuhamia Zanzibar kwa kuhamisha mtaji wake na biashara zake rasmi kutoka nchi ya Oman na Mascut ambapo alikuwa akifanyia biashara lakini pia alipokuwa akitawala baada ya kuwa na sintofahamu na ndugu yake huko Oman katika ufalme.

Ndipo Sultan Seyyid Said akaamua kufanya makazi rasmi Zanzibar huku akijishughulisha na biashara ya Uuzaji watu (slave trade) ambayo ilikuwa imeshamiri kipindi hicho, na Zanzibar ndio ilikuwa ndio soko kuu la watumwa kwa upande wa Afrika Mashariki. Baada ya misafara mbalimbali ya caravan ambayo walibeba pembe za ndovu na bidhaa zingine muhimu ikiwemo madini kama vile dhahabu, shaba, chuma na binadamu, walifikishwa Zanzibar na baadae kuuzwa kwa Mataifa ya Ulaya na bara la Asia.

Sultan aliwanyima haki wanawake wa Zanzibar kwani hawakuruhusiwa kumiliki mali, hawakuruhusiwa kusoma na kupata elimu, hawakuruhusiwa kwenda sokoni au kufanya jambo lolote sawa na mwanaume.

Huku wanaume pia waliadhibiwa na kuwabeba masultan hao kiasi kukosa uhuru wa kuabudu, kumiliki mali na hata kutoshiriki katika masuala ya kisiasa kwa kuto wapatia haki ya kuchagua ama kuchaguliwa katika nafasi yoyote ya kiuongozi jambo ambalo watu wenye asili ya kiasia, kihindi na wazungu ndio waliopewa Haki hiyo.

Kutokana na hali hiyo vuguvugu la kuiondoa Serikali ya kihafidhina ya kisultani nchini Zanzibar ikaanza kwa kuanzishwa vyama mbalimbali kama vile ZPP, ASP, na vyama vingine ambapo awali vilifanya harakati zake kwa siri siri na baadae chama cha ASP kikiongozwa na hayati Sheikh ABEID AMANI KARUME waliweza kuongoza mapinduzi hayo tarehe hiyo ya 12.01.1964 ambapo hadi leo yanakumbukwa kwa namna walivyoweza kumsaidia Mzanzibari kuweza kumiliki uchumi wake binafsi, kuabudu, kupata elimu kushiriki masuala mbalimbali ya kisiasa kwa kuchagua viongozi wanaowataka na pia kuwa na haki ya kuchaguliwa.

Vile vile wanawake wakaanza kuwa huru na kukawa na usawa wa kijinsia kwa wanawake na wanaume na hata wao kushiriki ujenzi wa Nchi na uchumi kwa kufanya kazi, biashara na Shughuli nyinginezo.

Hali hiyo ilipelekea wana Malenga maarufu kama Ali Marhum Skeikh Daktar SEIF KHATIBU kuandika Diwani mbalimbali za kuelezea historia ya Zanzibar na Mapinduzi matakatifu kama vile diwani ya WASAKATONGE, FUNGATE YA UHURU pia wanamalenga wengine waliandika mashairi kama vile HINA INAPAPATUKA, N.K
ambapo mashairi haya yote yaliweza kuelezea hali ya awali ya Zanzibar ilivyokuwa ya kimfumo dume na kiunyanyasaji hata kabla ya kupata uhuru, sasa Zanzibar ipo huru inawapa fursa kila Mzanzibari kuweza kuijenga Zanzibar hasa KUPITIA UCHUMI WA BLUU ambao Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt HUSSEIN MWINYI ametambulisha na unaonesha mapinduzi chanya kwa kuifanya Zanzibar Kuwa ya kisasa na inayopiga hatua kubwa ya kiuchumi na kimaendeleo.

Hii ndio faida ya Mapinduzi haya Matukufu Zanzibar, ambayo tunayaenzi na kuyaadhimisha kwa kuwapa kongole mashujaa wetu wote waliojitoa mhanga kwa ajili ya sisi wengine tupate kukomboka.

Tangu mwaka huu 1964 Zanzibar imeongozwa na maraisi 8 hadi sasa huku wa kwanza akiwa ni
1.Hayati Sheikh ABEID Amani Karume -1964-72
2. Sheikh Aboud Jumbe -1972-84
3. Ali Hassan Mwinyi-1984-85
4. Idris Abdul Wakil -1985-90
5. Salim Amour 1990-2000
6. Dkt Amani Abeid Karume-2000-2010
7. Dkt Ali Mohammed Shein-2010 -2020
8. Dkt Hussein Ali Hassan Mwinyi 2020-

Ndipo Wanzanzibar waliamua kutunga wimbo Maalumu wa kuyaenzi na kuwakumbuka mashujaa wote wa Zanzibar ambao wakipigania uhuru huu na wimbo huu unajulikana kama WIMBO WA MASHUJAA WA ZANZIBAR UNABETI KAMA IFUATAVYO. Nami leo najiunga nao kwa furaha kabisa kuuimba tunapoelekea kuadhimisha miaka 58 ya Mapinduzi haya Matukufu

1.Sisi sote tumegomboka ,kwa ndugu zetu waliopotea ×2
Walopigania nchi yetu, makusudi ya kuligomboa,×2
Hatusahau maisha yetu, kwa roho zao walozitoa×2

2.Ndugu zetu wamepotea, kwa kugombania nchi yetu×2
Mhanga wao wamejitoa ,kwa kulilinda wa Taifa letu×2
Hatusahau maisha yetu ,kwa roho zao walozitoa×2

3.Hao ndio walimu wetu, waliokwisha kujitolea ×2
Na sisi hatutarudi nyuma, sote mbele tutaendelea ×2
Kwa kulilinda taifa letu,mhanga sote twajitolea ×2

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %