0 0
Read Time:3 Minute, 45 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
February1,2022.

Asanteni Ikulu kwa kunisikia kwani mwaka huu January 1,2022 niliandika Makala yenye kichwa cha habari kinasema”Je,Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu IPO usingizini?”.Leo tena February 1,2022 mwezi mmoja tu tangu niandike makala ile,ndugu zangu pale Ikulu walishaona udhaifu ambao na mimi nilishauona na kuuandika zaidi ya mara tatu nyuma!

Nianze kwa kusema kuwa, taasisi hii ya Urais na Mh.RAIS mwenyewe,sio tu kwamba inapaswa kulindwa kwa silaha za moto pekee dhidi ya maadui wa Taifa, lakini pia Mh RAIS anapaswa kupewa ulinzi wa kiakili,kiroho na hata kiafya ili aweze kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kikatiba.

Mheshimiwa Rais akikosa utulivu wa kiakili yaani “mental stress”ni wazi kuwa atashindwa kutekeleza majukumu yake ya kila siku hivyo malengo ya TAIFA yanaweza kutofikiwa.

Ndio maana wakati mwingine kazi hizi nyeti kama za Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,zinahitaji mtu ambaye ni zaidi kujua uandishi wa habari ambaye labda anafahamu nini maana ya kuilinda na kuikuza brandi nzima ya urais na kuweza kukubalika mbele za watu wote!Rais ni kama bidhaa na mwisho wa siku iwe mbaya iwe nzuri, lazima hii iweze kuuzika sokoni!Period!

Bahati mbaya sana mamlaka za uteuzi zinadhani kwamba, mwandishi yoyote wa taaluma ya habari,anaweza kuifanya kazi hii bila kupwaya na hapo ndipo tunapokosea!

TANGIA kuzuke mjadala wa Serikali kukopa kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo na hatimaye Mh Rais kupata upinzani wa wazi kutoka mhimili mwingine za dola,si Msemaji wa Serikali wala si Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ameweza kusimama na kujibu hoja kwa lengo la kumlinda Mh.Rais wetu asichafuliwe dhidi ya shutuma hizo!

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali,always wanapaswa kuwa “cover” ya Mh. Rais kabla hajafikiwa na Mtu au kitu chochote kile!

Wakati mwingine unaweza ukaona udhaifu wa Serikali kwa haraka haraka kutokana tu na kukosekana kwa watu wenye weledi wa kuilinda taasisi ya urais na RAIS mwenyewe lakini pia unaweza “ukanote” uimara wa Serikali au taasisi ya urais kutokana na kuwepo watu wenye weledi na umakini wanajua jinsi ya kuitengeneza na kuilinda taasisi ya urais kupitia mawasiliano ya kimkakati!

Haiwezekani taasisi ya urais iwe inashambuliwa mchana kweupe huku watetezi wake Mh Rais wakawa wapo kwenye usingizi mzito huku wakiwaacha watoa “nongwa” wakitamba usiku mchana katika majukwaa yao mbalimbali ya habari,huku wenyeviti wa CCM Mikoa ndio wakibeba jukumu la kumpambania na kumlinda huku watu wenye taaluma zao wakiwa wapo kimya KABISA maofisini!

JE BI ZUHURA YUNUS ANA SIFA HIZI NILIZOWAHI KUZITAJA?

1.Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu lazima awe na akili kubwa kuweza (I)kusoma kwa haraka sana lengo la ndani mtoa hoja(Ii)kusoma kwa haraka public upinions inasomaje kuhusu hoja husika(iii)na kuweza “kuconsolidate” taarifa ya haraka na
kujibu hoja husika kwa nidhamu,usahihi na takwimu za wazi kuhusu hoja husika!

2.Uwezo huu wa mtu ambaye anatajwa kuweza “kuzicontain”(I)hoja ya mtoa hoja(Ii)na kusoma na kutafsiri public opinions kwa haraka ndio uzaliwa watu wanaitwa “spin doctors” kwenye mawasiliano ya kitaasisi!Hawa ni watu maalum wenye taaluma zaidi ya moja ambao chakula chao cha kila siku ni taarifa taarifa taarifa!

3.Gusa popote unapotaka kugusa kuhusu taasisi ya urais,watu hawa watakujibu kwa usahihi na kwa utulivu mkubwa huku wakiwa wanatabasamu na mwisho mhusika(hoja) anaishia kukubaliana nao hivyo kuifanya taasisi ya urais na RAIS kuweza kung’ara kila siku!

4.Kwa TAIFA kubwa kama Marekani, watu hawa “Press Secretary” uandaliwa kwa muda mrefu kuja kuchukua majukumu haya mazito!Umeona na unamkumbuka Msemaji Mkuu wa Serikali ya Sadam Hussein wa Iraq wakati wamerkani wanaingia Bagidad?

Uwezo wa kumlinda Rais wetu dhidi ya propaganda mpaka siku ya mwisho ndio sifa kubwa ya spin doctors!

5.Sitaki kumsemea vibaya Dada yangu ZUHURA YUNUS lakini bado naona tunarudia makosa yale yale katika teuzi hizi nyeti!

Mkurugenzi wa Rais Ikulu sometimes anatakiwa kuwa “smart” zaidi ya taasisi yenyewe anayoisemea!

Wale tulicheza mpira wa miguu tunajua majukumu ya sweeper” au “kitasa”!Unapokuwa na viungo wanaofanya makosa then kazi ya “sweeper” ni kufuta makosa!

6.Zaidi ya yote Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais lazima awe na uwezo wa juu wa “kucommand issues’!Je,Huyu ndio ZUHURA YUNUS?👏🏽👏🏽👏🏽

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani Mawasiliano ya Umma,Chuo Kikuu Saut & Tumaini Iringa na Mtia Nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255746726484.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %