0 0
Read Time:2 Minute, 47 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
February 2,2022.

Ni wazi kuwa mabadiliko yoyote katika jamii ya watu ni hatua yaani “gradual process” na mabadiliko sio tukio”an event”!Ukitaka kuyafanya mabadiliko ndani ya taasisi au jamii kuwa tukio kwa maana ya kuyafanya kwa siku moja kuna mambo mawili yanaweza kutokea(i)ukubali kukutana na kitu kinaitwa “resistance to change(ii)au the performance failure!

Mimi ni mmoja wa waumini wakubwa wa dhana nzima ya usawa wa jinsia katika maeneo yote lakini wasiwasi wangu ni kwamba njia tunazotumia kufanya “gender balance” zinaweza zikaja “kubackfire” dhidi ya CCM mwaka 2025 kama tusipokuwa na mkakati makini wa kuweza kuziweka sawa!

Ni ukweli kuwa wakati jinsia moja imekuwa ikipeta katika nafasi za uteuzi kuna jinsia upande mwingine ni kama inapigwa na bumbuwazi japo hawasemi hadharani lakini bumbuwazi hiyo ipo tena ni kubwa mno!

Political researchers & strategists wa ccm hawapaswi kuogopa kumshauri Mama kwani huo ndio wajibu wao kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na taasisi nzima ya CCM kamwe hawapaswi kuukwepa!

Kwa jicho langu naona ni wazi kuwa CCM mwaka 2025 kuelekea Uchaguzi mkuu, tunaenda kumtengeneza adui wetu wenyewe ndani ya chama na anaweza kuja kutusumbua sana”gender class struggle within CCM”.SIJUI kama jicho langu linaona vizuri sana!

Tukiimaliza vita hii”Men vs Women” ya ndani ya CCM yetu kiusalama, tutakwenda kukutana na shida hiyo hiyo nje ya CCM dhidi ya vyama vya upinzani na dhidi ya wananchi hasa wapiga kura wetu!

KWANINI AJENDA HII INAWEZA KUPUNGUZA KURA ZETU CCM MWAKA 2025?

1.Ajenda hii ya usawa wa jinsia sio ajenda mpya kabisa katika Taifa lakini je,jinsia ya pili iliandaliwa kukubali mabadiliko haya ya gafla kiasi kwamba isije ikaona kwamba hii ni vita ya kutafuta nafasi za uongozi baina ya jinsia mbili?

2.Je,tuna programu gani huku chini za kuweza kuwaanda wanawake mashuleni au vyuoni au ndani ya jamii zetu kwa ujumla ili kuweza kuwafanya wakubalike na kuchagulika katika ngazi za chini za maamuzi?Kwa maoni yangu,CCM ilipaswa kupima upepo huu wa jinsia ndani ya chama kuelekea uchaguzi wa ndani wa CCM yenyewe mwaka huu!”gradual process”.

3.Ni wazi kuwa ajenda kubwa ndani ya uchaguzi mkuu wa CCM mwaka huu itakuwa ni wanawake dhidi ya wanaume hivyo kuweza kuleta mpasuko ndani ya chama!Wanaume lazima waambiwe sasa na kuwekwa sawa kisaikolojia kwamba hii sio vita!

4.Ni wazi kuwa idadi ya wanawake katika nafasi nyeti katika Taifa ilikuwa ni ndogo Sana!swali ni je,unawezaje kuziba pengo hilo na hapo ndio pana mtihani mkubwa!”gradual process vs evental”.

5.Mh Rais na Mama yangu Samia Suluhu Hassan, anapaswa kushauriwa vizuri zaidi katika kuliendea hili ili kuepuka “gender class struggle” ndani ya CCM na dhidi ya vyama vya upinzani!

Ni wazi kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa CCM mwaka 2025 kisimamisha wagombea wengi wakina Mama katika majimbo hivyo nafasi walizokuwa nazo wanaume kupotea.

Vyama vya upinzani vinaweza kutumia mwanya huu “kubet” kwa kisimamisha wanaume katika majimbo!unajua nini kitatokea?ni wazi kuwa wale watia Nia wa CCM ndani ya CCM ambao watakuwa wamekosa nafasi wanaweza kuja kuwa mwiba kwa wagombea wetu!

Kazi yangu ni kushauri tu njia bora ya kuweza kufikia usawa wa jinsia na niseme wazi kuwa Mimi ni muumini wa usawa wa jinsia haswa!Wale wanawake mlioaminiwa na Mh.Rais msije kumwangusha!

https://global.chinadaily.com.cn/a/202104/01/WS6065245ca31024ad0bab2f37.html

+255746726484.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %