0 0
Read Time:53 Second

WU® MEDIA

Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr Hussain Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa Italy Mh. Marco Lombardi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameupongeza utayari wa Serikali ya Italia kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji wa mipango yake ya maendeleo.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo leo Ikulu Zanzibar katika mazunguzo kati yake na Balozi wa Italia nchini Tanzania Marco Lombardi, Ikulu Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Mwinyi alipongeza azma ya Serikali ya Italia ya kushirikiana na Zanzibar katika kuhakikisha inaimarisha sekta zake za maendeleo ikiwemo sekta ya utalii ambapo nchi hiyo ni mdau mkubwa.

Rais Dk. Mwinyi alifahamisha kuwa Zanzibar kwa kipindi kirefu imekwua ikinufaika kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wawekezaji na wageni kutoka nchi ya Italia.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alimuahidi Balozi Lombardi kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuweka mazingira mazuri katika kuhakikisha wawekezaji na wageni wanaotoka nchi hiyo pamoja na nchi nyengine duniani wanatekeleza shughuli zao katika mazingira yanayokidhi matarajio yao.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %