0 0
Read Time:1 Minute, 2 Second

WU® MEDIA

28/02/2022
 

ARUSHA
Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumatatu, Februari 28, 2022) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu. Mkutano huo unafanyika jijini Arusha.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kwama Serikali ya Tanzania ipo tayari kuwapokea na kushirikiana nao pale watakapohitaji ushauri wa aina yoyote. Mkutano huo umefunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria Prof. Yemi Osibanjo.
Amesema Mahakama hiyo ilianzishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kusimamia haki za binadamu, ambapo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia alipata fursa ya kueleza dhamira ya Tanzania katika kuunga mkono jitihada za mahakama hiyo kufanya kazi.
Naye, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria, Prof. Yemi Osibanjo akizungumzia kuhusu ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika inayolenga kulifanya Bara la Afrika kuwa bara lenye nguvu duniani katika siku zijazo amesema kuwa ipo haja ya kutambua changamoto zinazokabili Bara la Afrika ili waifikie Afrika wanayoitaka.
 
Ameongeza kuwa ni muhimu kuangalia namna ya kutafsri yote yaliyoanishwa kwenye agenda 2063. “Lazima tutumie fursa na taasisi zote tulizonazo ili tuweze kufikia Afrika tunayoitaka lengo ni kuhakikisha tunaona maisha ya Waafrika yanaboreshwa na uchumi unakua.”

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %