0 0
Read Time:51 Second

WU® Media PRODUCTION

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa ujio wa Rais wa Shirikisho la mchezo wa kuogelea duniani (FINA) hapa Zanzibar utasaidia kwa kiasi kikubwa kuitangaza Zanzibar kiutalii hasa katika utalii wa michezo.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo alipokutana na Rais wa Shirikisho la mchezo wa kuogelea duniani (FINA), Hussain Al Musallam akiwa na ujumbe wake wa viongozi mbali mbali wa Shirikisho hilo kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwemo waliotoka Makamo makuu ya (FINA) nchini Switzerland.

Katika mazungumzo hayo Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa mchezo huo ni maarufu duniani na ujio wa kiongozi huyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Zanzibar na Shirikisho hilo la mchezo wa kuogelea duniani (FINA).

Aliongeza kuwa hatua hiyo itaisaidia sana Zanzibar ambayo imezungukwa na bahari, na kwa vile imo katika mikakati ya kuimarisha Sera ya uchumi wa Buluu ambapo miongoni mwa malengo iliyojiwekea ni kuimarisha sekta ya utalii kwa kupitia utalii wa michezo.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %