0 0
Read Time:1 Minute, 13 Second

WU®Media PRODUCTION

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
March 25,2022.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan unaweza ukadhani hatembei kumbe ndio anakwenda hivyo kuelekea mwaka 2025 na mwisho wa siku mkija kumkagua, yeye atakuwa kashamaliza kazi zamani!

Kwa wale tuliocheza mpira wa miguu tunajua kuwa kuna wachezaji ambao hawatajwi na kutazamwa sana na washabiki lakini wana madhara na michango mikubwa kwa timu zao katika kupata ushindi!Pale Simba kuna Mzamiru Yassin na pale Yanga kuna Feisal Salum!Kila siku utamsikia Mayele au Chama basi!

Mwaka mmoja tu tangu kifo cha mtangulizi wake hayati JPM,Mama Samia ni kama hana papara na wala hayumbishwi na maneno ya mitaani kuhusu utekelezaji wa miradi yote waliyoanzisha yeye na mtangulizi wake!

Ndani ya mwaka mmoja wa utawala wake,tayari Mama Samia kashachukua na kuweka pointi mbili muhimu,moja kaibeba kupitia uzinduzi wa nyumba za makazi magomeni kota na pointi ya pili kaibeba kupitia daraja la Tanzanite zamani Salender!Ndani ya wiki moja Mama Samia kashachukua pointi mbili safi kabisa!

Nani ambaye anaweza kusema kwamba Mama Samia hatoweza kukamilisha miradi yake mpaka hapa?

Ni ngumu kuamini kuwa mpaka sasa Mama Samia Suluhu Hassan ameshaokota pointi mbili safi kabisa!Jamaa wanaweza kupoteana mapema sana!

Kipande cha SGR kutoka Dodoma- Tabora -Kigoma kimeshaanza kujengwa 2022 hii!Inawezekana sana miradi yote ya kimkakati ikaweza kukamilika kabla ya mwaka 2024.Dah,Mama “anatembea” sana!

Bora tufunge midomo kabla hatujaumbuka kuelekea mwaka 2025!Kama mnabisha,sawa!

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %