0 0
Read Time:2 Minute, 38 Second
JICHO LA ULEDI

George Michael Uledi.
Kyela,MBEYA.
March 29,2022.

Ni Binti mzuri na mrembo mwenye kila kitu Afrika Mashariki, ameingia rasmi ukumbuni huku mbele yake kukiwa na “njemba” sita zikimtazama!JE,nani anaweza KURUDI nyumbani na Binti huyu?kwangu linabaki kuwa swali muhimu kwa wachora ramani ya uchumi-jasusi ndani ya jumuiya ya Afrika mashariki yaani Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda,Burundina Sudan Kusini!

Binti Congo ana idadi ya watu ya 90 milioni mpaka leo mchana huu,hili ni soko kubwa la chakula na bidhaa kutoka ndani ya Afrika mashariki!Binti Congo ni tajiri wa madini ya kila aina!Binti Congo kwa kutumia misitu yake anaweza kukupa utajiri wa biashara ya mbao kwenda nje!Majirani mnataka Nini?Binti Congo ana kila kitu nimetaja vichache!

Nimeamua kutumia lugha ya picha angalau kumwelezea na kuwatia njaa “watu wetu” ambao ndIo maplanners na strategists” wa kumshauri Mama Samia ya jinsi ya kuvuna utajiri nje ya mipaka yetu!Kama hatuna idara au kitengo maalum cha namna hii au tunacho lakini kama tumekipa kisogo kidogo basi tunapaswa kesho tukiamshe haraka kwa ajili ya maslahi mapana ya TAIFA langu Tanzania!

Si ndio leo Nchi ya Congo ya DRC inaingia rasmi ndani ya jumuiya yetu ya Afrika mashariki?swali langu hapa JE,tumeshachora ramani sisi kama Tanzania ya kuyatafuta maslahi yetu ya kiuchumi ndani ya Congo haraka?,JE,tuna taarifa za mipango ya jirani zetu wote sita KUHUSU mipango yao ya siri kuhusu Congo?(kiuchumi,kiusalama na mingineyo), Lazima tuwe na taarifa muhimu zote kuhusu mipango ya jirani zetu kuhusu Congo mapema wakati huu wacongo wanajiunga kwenye kuelekea shirikisho letu la Afrika mashariki!

Kwa kuonyesha kwamba Kigali wapo na njaa “aggressiveness”kiasi gani, tayari Paul Kagame na Rwanda yake wameshafanya majaribio kadhaa ya kukaa ndani ya Congo na kwa sasa watakuwa kama wamepata kibali rasmi cha kutekekeza maslahi yao kwa haraka ndani ya Congo!

Tanzania tuna advantage moja ya kumpata “Binti- Congo” na wakongo wanajua kuwa, sisi Tanzania ndIo watu wenye ushawishi na heshima KUBWA ndani ya ukanda huu wa Afrika mashariki kuliko Nchi nyingine!Nani anabisha?

Natamani Stamico wangekuja na Proposal yao mezani na wamwambie Raia namba moja wetu, Mh Rais Samia Hassan kwamba sisi kama Shirika la madini la Serikali tunataka kwenda Congo kuyatafuta maslahi ya Nchi!

Then wamsikie Mama yetu na Rais wangu anasemaje!Lazima Mama yangu ashawishiwe na strategists wetu kwamba hakuna namna ambayo tunaweza “kutoboa” bila kutoka nje ya mipaka na kwenda kwa majirani zetu dhaifu!sisi ni TAIFA kubwa lazima tutumie mbinu za “kibabe,kificho na za wazi” kuyatafuta maslahi yetu usiku na mchana nje ya mipaka yetu!

Sisi hatuwezi kuwa watazamaji kamwe wa uchumi wa kimataifa!Kigali mpaka sasa kashafanikiwa kufungua “Gold Refinery Plant” pale Rwanda, target kubwa ikiwa madini ya kutoka Nchi ya Congo,kumbuka Paul Kagame hana hata “PIT” moja ya dhahabu zaidi ya kuwa na njaa ya maendeleo tu. “aggressive tu’

Kila mtu Serikalini na wafanyabiashara waanze kufikilia jinsi ya kumkamata “Binti Kongo” kuanzia sasa!Sisi Tanzania tuna uwezo wa “kuupset” yoyote tukiamua hata sasa!Rwanda,Kenya Uganda, Burundi na Sudan Kusini sio lolote kwetu!Sisi ndIo “Giant ” hapa Afrika mashariki na lazima tukaonyeshe ukubwa wetu now now Congo!

Sijui naelewekaaa??

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %