

WU® Media PRODUCTION LIMITED
George Michael Uledi.
KYELA,Mbeya.
April 11,2022.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ndie RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan hivi karibuni anatarajia kuitisha KIKAO maalum cha CCM na MAWAZIRI wake, tangazo hili likitolewa rasmi jana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa,Afande Kanali Abdulhman Kinana(rtd)!
Lengo la kikao hicho maalum na muhimu, pamoja na mambo mengine ni kuweza kujadili hali ya ugumu wa maisha inayowakabili watanzania kwa sasa,Mh.Afande Kinana alinukuliwa akisema!Kwanza nampongeza Mh.Mwenyekiti wangu wa Chama,Mh.Samia Suluhu Hassan kwa kutambua uwepo wa ugumu wa maisha hasa kutokana na uwepo wa mfumuko mkubwa wa bei kwa zile bidhaa muhimu”inflation”.
Hili ni bonge la gori zuri ambalo Afande tactician wa siasa- mkakati,Comred Kinana ameanza kulifunga tangu achaguliwe kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa wiki kadha zilizopita!Hongera Mh.Rais kwa kutambua uwezo wa Afande Kanali Kinana!
MASWALI YANAYOUMIZA KICHWA CHANGU KUELEKEA MKUTANO HUO NI HAYA HAPA!
I. Ni wazi kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa ndie RAIS wa Jamhuri ya Muungano na ndie Mkuu wa Serikali!If so,Je,Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa anaweza kujihoji mwenyewe kuhusu ajenda ya ugumu wa maisha hasa uwepo wa inflation ya kiwango cha juu katika Nchi?
Na hapa ndipo suala la kofia mbili linakosa uzito kwa upande mmoja katika kutekeleza suala la “check & balance” baina ya CCM kama Chama dola DHIDI ya Serikali!Mwenyekiti wa CCM angekuwa na nguvu sana katika kikao hiki kama angekuwa sio RAIS na Mkuu wa Serikali mwenyewe!
II. Ni wazi kuwa baadhi ya MAWAZIRI wangu ndio sehemu ya(tatizo) ugumu huu wa maisha ya watanzania either kwa kushindwa kuratibu vizuri mipango ya Serikali ndani ya wizara zao na hatimaye kuleta unafuu wa maisha kisekta mfano sekta ya Nishati na mipango-uchumi au kwa kushindwa kumshauri vizuri Mh RAIS kuhusu maeneo yao ya kisekta wanayoyaongoza!
Je,MAWAZIRI wangu watapata wapi AKILI kubwa mpya kwenye kikao hiki ya kuweza kumshauri Mh RAIS kuhusu majibu ya matatizo ya watanzania kama wao ndio sehemu ya matatizo hayo?
Rejea Press Conference ya mbunge Luhaga Mpina(Mb)kuhusu Wizara ya Nishati na pia rejea mchango wa Mh.Tabasamu Bungeni juzi kuhusu Wizara ya Nishati lakini pia rejea mchango Mh.Aboud Bungeni kuhusu Wizara ya Nishati!
III. Ni wazi kuwa Ilani ya uchaguzi ya CCM imeelekeza nini cha kufanya,wapi pa kufanya na lini tufanye!Mpaka sasa Chama CHANGU ingebidi kiwe na majina mkononi tayari ya kuingia nayo kwenye kikao hicho na kumshauri Mkuu wa Serikali na Nchi kuhusu kufuta uteuzi wa baadhi ya MAWAZIRI ambao mpaka sasa imeonekana wazi wameshindwa kutekeleza Ilani yetu ya uchaguzi ya 2020/2025.
Je,CCM ya Afande Kinana itakuwa na ubavu wa kufanya haya?matarajio yangu kuhusu kikao hicho yangekuwa na impact kubwa na kuweza kubadili siasa za NDANI ya CCM kama mambo haya yangeenda kutokea kwenye Mkutano huo na zaidi, yangeongeza heshima ya dhana ya kofia mbili kwa maana ya RAIS wa Jamhuri ya Muungano na hapo hapo kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa!Kuna sehemu dhana hii inakosa nguvu kabisa!
IV. Ni wazi kuwa Chama CHANGU kitaenda kuielekeza Serikali ya CCM kuhusu nini cha kufanya!Wasiwasi wangu ni Je,tangia lini CCM ikaweza kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu masuala ya mkwamo wa uchumi kwa mfano?
Au CCM kitaenda kusikiliza mipango ya MAWAZIRI wangu kuhusu jinsi gani tunaweza kutoka katika mkwamo huu wakati watu hao hao kwa njia moja au nyingine ndio sababu ya kuwepo kwenye mkwamo huu wa sasa!
V. Kwa maoni yangu,CCM ilipaswa kuwa na kikao kama hiki na “Think Tank” wa uchumi kwanza kabla ya kuwageukia MAWAZIRI wake hawa!Hii ingesaidia kukipa Chama picha kubwa ya nini kinaendelea duniani hivyo kuja na majibu yenye picha kubwa hivyo wangeweza kuwabana vizuri zaidi MAWAZIRI kwenye kikao chao na watu hawa!
Natamani kikao hiki kati ya CCM na Mawaziri wake kingeenda kuwa kikao cha maelekezo zaidi kuliko kuwa kikao cha majadiliano kwa lengo la kuweza kuresque situation kwa haraka zaidi ukizingatia wabunge wangu wameshaanza kupiga positive kelele mjengoni!
Wajibu wangu kama kijana wa CCM na kijana wa kitanzania ni kuwaza hivyo kuweza kuchochea fikra mpya za kuweza kuisukuma Tanzania yangu mbele zaidi na zaidi!
Kazi hii ntaendelea kuifanya kwa ufasaha mkubwa kwa maslahi ya Chama changu CCM na kwa maslahi ya Taifa langu Tanzania!
+255784159968.









