
WU Media PRODUCTION LIMITED
WAMEAMZA KUVIMBA MAPEMA KABISA!
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
April 11,2022.
Moja ya teuzi ziliwahi kuleta kelele ndani ya CCM na kwa watanzania kwa sasa ni utuezi wa Braza yangu comred Nape Mnuye,waziri wa Habari wa sasa mpaka kupelekea uwepo wa mijadala ya “wamerudi tena” kwenye social media nyingi nchini!

Kaka yangu, Mwalimu mwenzangu na kada mwenzangu wa CCM,Thadeo Ole Mushi leo kapinga wazi wazi matumizi ya Chopa ya Mh. waziri Nape kwenda kuhamasisha zoezi la anuani za makazi Nchi nzima!Huko kwenye social media watanzania wamejifungia wakicheka na kishangaa nini kinatokea kwa sasa!
Huwa mi najiuliza kweli Serikali hii ya CCM haina watu “wanaomonitor” public opinions kwenye “main stream & social media” na mitaani kila siku kujua “how do people perceive their government” na kufikisha TAARIFA hizi muhimu kwa Mama yangu Samia angalau achukue hatua!Je,kama watu hawa wapo Je,wanamwambia Ukweli kweli?I worry!
Nimefundisha Chuo Kikuu somo la “Public Opinions & Perceptions” angalau miaka mitano hivi,najua ninalosema!Ni HATARI sana kwa Serikali yangu ya CCM kupuuza kitu kizito kinachoitwa Public Opinions & Perception kwani hata mashirika ya KAWAIDA hayajawahi kupuuza UTI wa mgongo huu wa kuendesha Nchi!
Zoezi la Anuani za makazi hapo kabla lilitengewa mabilioni mengi ya fedha zaidi ya Billioni 100 kama sijakosea na Bajeti ile ilipofika mezani kwa Mh Rais, Mama yangu Samia,yeye akayafyekelea mbali na kubakiwa na Vibilioni vichache kwa lengo la kubana matumizia ya Serikali”cut cost government”!
Wakati Mh Rais alikuwa na lengo la kupunguza gharama,Mh waziri Nape anakumbuka na pia kama kamis maisha ya kutumbua ya awamu ileeeeee!Nasikia Leo kaamua kufungua milango ya Chopa na kuzama ndani!
Wakati Watanzania wenzake Mimi, wewe, PAMOJA na kaka yangu Thadeo Ule Mushi japo tuna vidigree vyetu vingi makabatini,lakini hatujawahi KUVIMBA angalau kwenye V8 hata siku moja!
Kaka yangu Waziri Nape ameshapita huko kwenye level za V8,yeye anawaza chopa chopa chopa!Nchi bwana ukishaipatia!Khaaa!
Gharama za kuizunguka Nchi nzima kwa Chopa sijui ni Balioni mangapi lakini angalau niseme ni gharama kubwa na ile dhana ya cut cost ya Mama kuhusu Bajeti ya zoezi ili ni kama Nape ameipuuzaaa!
Mwakani tuna zoezi la Sensa ya Watu na Makazi!Natarajia kwa style hii Mh.Waziri wa fedha kaka yangu Mwigulu nae pia anaweza kuota kuitaka chuma ya chopa kwenda kuhamasisha zoezi hili muhimu la Sensa ya Watu na Makazi Nchi nzima!Mpaka sasa hatuna uhakika na Bajeti ya fedha ya Sensa,badala la kujibana kutunza kidogo kilichopo sisi tunatumbua!
Nakumbuka Dada yangu Dr. Merry Mwanjelwa mwaka 2018 mpaka 2019 aliweza kuizunguka Nchi nzima ya Tanzania kwa V8 tu katika kuhamasisha utekelezaji wa mpango wa TASAF kwa kaya masikini, nadhani wakati ule Dada yangu Merry angetangaza kuitaka kutumia chopa lazima nina uhakika “Simba wa Yuda angeshamlalua” lakini!Mama kusema ukweli wateule wako wanatupa wakati mgumu mno wa kusema mazuri ya Serikali yako!Wakati mgumu Mno,Mno,Mno!
Ni bora tutengeneze nidhamu ya uoga kwa mawaziri na watendaji ambao wanashindwa kujisimamia wenyewe kuliko kuendelea kuwapa nafasi ya kujisimamia wakati hawana uwezo wala utashi wa kujisimamia!
Watu wa kitengo vya Habari please msaidieni Mama kujua ukweli wa haya!Hii Habari ya kumdanganya danganya hapana hapana!Juzi tu mmetoka kumtia aibu kipenzi chetu!
Nchi inapaa na kusonga mbele,ninyi mnakuja na data zenu fake kuhusu kwamba Tanzania imetolewa kuwa NCHI YA UCHUMI WA KATI,Hivi watendaji mna nia gani na Serikali ya CCM?,inaonekana watu wamerelax sana!Jamani Rais wangu kila siku anasema na hapa namnukuu;
“….Kuna vijana wengi mko mtaani wenye sifa na wanazitaka nafasi hizi…”na tunazitaka kweli,endeleeni kuzichezea!
Msemaji wa Banki ya Dunia ambao ndIo watoa takwimu rasmi za Kila mwaka za nafasi ya Nchi zetu kiuchumi, juzi wamekuja na kuweka data SAWA kuwa Tanzania is still katika kundi la Nchi zenye “UCHUMI WA KATI”.Why this?
Juzi Juzi niliandika Makala na kidogo kuwastua wakina kaka yangu Bakari Machunu wa MCL na kaka yangu Mwigamba, sijui kama bado yupo The Guardian bado kwamba Magazeti yao yamekuwa kama “toothless dog”!Hivi suala lile”kuondokewa kwa Tanzania kwenye uchumi wa kati” baada ya kauli ya Mh.Rais lingepitaje hivi hivi bila kujadiliwa kama tungekuwa na vibrant media?
Mh.Waziri Nape achana na mpango wa Chopa,Mama yangu Samia kamwe ukimya na busara yake msimchukulie kama ndIo udhaifu wake!Sisi vijana wa CCM kama Mimi Uledi na Ole Mushi tutasema kwa niaba ya Mama maana vijana wenzetu wa CCM wanaamini kukaa kimya ndIo uteuzi utakuja haraka kwao!Bora kukaa nyumbani kuliko kukaa kimya!
+255784159968.








