0 0
Read Time:55 Second

WU®Media PRODUCTION LIMITED

MTANGANYIKA WA KWANZA KUWA MEYA.

Je wajua asili ya jina la Uwanja wa Sheikh Amri Abeid linamuhusu nani?

Alikuwa Mwanasiasa na mshairi, pia Msomi wa dini ya Kiislam. Alizaliwa mwaka 1924. Alikuwa Meya wa Kwanza Mwafrika katika historia ya Nchi ya Tanganyika (Tanzania) alikuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Kama ilivyokuwa kwa Wanazuoni wa islamu wengi ambao ndio walikuwa vugu vugu la kudai Uhuru , na wakawashirikisha wanasiasa wengine wa madhehebu tofauti tofauti miongoni mwa walioalikwa kuungana nao kudai Uhuru ni Mwalimu Nyerere, huyu pia alikua na urafiki na Nyerere, Chanzo cha Waislam kudai Uhuru ni kutokana na wao kuhisi kuathirika zaidi na ubaguzi wa Elimu na ajira na hila nyingine katika haki wakati wa Ukoloni.

Hapo ndipo walipoibuka kina Milambo, Mkwawa, Na Asili ya Vita vya majimaji ni hao hao masheikh.

Jina la Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo Arusha uliitwa Jina hili kuenzi mchango wa Huyu mwanasiasa. Kuna Uhusiano kati yake na Shule ya Msingi Kaluta iliyopo Ujiji Mjini Kigoma, ambako ndio Asili yake Sheikh Amri Abeid.

Mwenyezimungu Awape kheiri Wazee wetu waliojitoa kuhakikisha Leo tupo hapa .

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %