WU®Media PRODUCTION LIMITED
NI KWA NEEMA TU YA MH.RAIS MAMA SAMIA OTHERWISE WATUMISHI HAMKUSTAHILI BUMU HILI KWA SASA!
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
May 2,2022.
Pamoja na kwamba watumishi wa umma wa Tanzania hii wamekuwa mkitupiga “double double”yaani NJE NDANI lakini Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa,Mh Samia Suluhu Hassan bado anawapenda!Twapaswa tujitafakari dhidi ya upendo huu wa serikali ya CCM ya awamu ya sita kwenu!
CAG Kichere na Mh Rais, Mama Samia Suluhu Hassan mpaka sasa hajafuta machozi dhidi ya michuzi ambayo mmempiga kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 lakini bado unataka nyongeza!Ni ukweli kuwa michuzi ambayo CAG alitaja kupigwa ni wazi kuwa watumishi wa umma kwa namna moja au nyingine wanashiriki kuipiga!
Juzi juzi mmetoka kumpiga Mama Samia fedha yake ya mkopo ya COVID 19 kutoka WB lakini bado mnataka kumnyonya tena Mama Samia kama kupe!Tunajua kuwa huko mliko mnapata sana!Ingekuwa hailipi mngesepa kitambo!watumishi wa umma acheni kumzingua Mama!
Utendaji wa kazi wa watumishi wa umma ni kusuasua sana mpaka Mama Samia aliwahi kunukuliwa akisema kuna” lack of coordination” ndani ya utendaji wa Serikali lakini bado mnataka mama aongeze pochi!Kuweni na huruma basi kwa watanzania jamani!
Mzee wangu hayati JPM asingekubali hii,mna bahati sana watanzania na hasa wafanyakazi wa serikali mmepata Rais msikivu na serikali sikivu sana”responsive government”!
Kila kona Serikali hii ya CCM ni sikivu!Kwenye majukwa ya siasa ni majadiliano,kwenye majukwaa ya media majadiliano,kwenye mishahara tucta na serikali ya CCM ya AWAMU ya sita inasemekana walifanya majadiliano!
Huwa najiuliza kuwa hivi kwa mfano,Mh.Mama Samia Suluhu Hassan,Rais wa Tanzania na mgombea wa CCM nafasi ya Urais anashindwaje “kutoboa” mwaka 2025?Ni ngumu sana kumzuia Mama huyu kwa sasa ndani ya CCM na hata nje ya CCM.
Siasa zimekuwa rahisi sana wakati wa Mama Samia!Yaani CCM ya Mama Samia Suluhu Hassan inatumia akili kubwa kuliko nguvu kubwa na mambo yanasonga hatari!
Na hapa ndipo unapozaliwa ule msemo mtamu wa kitaaani yaani “MAMA ANAUPIGA MWINGI SANAAA”.
+255746726484.