
WU® MediaPRODUCTION LIMITED
Kazi Inaendelea nchini Italia katika Tamasha na Maonesho ya Kimataifa la Rimini MacFrut 2022, ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa Ikishiriki kikamilifu chini ya Uongozi wa Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Watendaji mbali mbali wa Ubalozi huo pamoja na Wizara ya Kilimo nchini Tanzania, Benki ya Uwekezaji na Mikopo katika Sekta ya Kilimo na Makampuni ya Biashara ya Kuchakata. Kufunganisha na Kusafirisha Mazao Kimataifa pamoja na Mboga na Matunda ya Eat Fresh ikiongozwa na Bi. Khadija Jabiri na Kaizen Logistics ukiongozwa na Bwana Brian Ngelangela wa Kaizen Logistics Exports kwa upande Maparachichi, Mboga na Matunda mengineyo ambayo nchi ya Italy ilieleza uhitaji wake. Afisa kutoka Wizara ya Kilimo anaeleza yafuatayo ambapo Tanzania pamoja na Ujumbe wake umefaidika katika Maonesho hayo ya Kimataifa ya MacFrut 2022 nchini Italia. Kazi inaendelea!








