
WU® Media PRODUCTION LIMITED
Rimini Italy
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mh.Mahmoud Thabit Kombo Leo ni siku ya pili ameendelea kushiriki kwenye Maonyesho ya kimataifa ya kilimo.
Mh Balozi katika siku ya Leo Pamoja na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali pia amepata muda wa kutembelea Mabanda mengine ya Maonesho ya Kilimo na Matunda ya Kimataifa “MacFrut 2022” yanayo endelea Mjini Rimini, nchini Italia.
Tanzania inawakilishwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Wizara ya Kilimo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, TAHA, Makampuni 8 kutoka Tanzania wakiwemo Eat Fresh inayoongozwa na Bi. Khadija Jabir na Kaizen Logistics inayoongozwa na ndugu Brian Ngelangela, Pamoja nao pia yupo Mjasiriamali wa Sekta ya Kulilimo Mama Kamugisha.
Miongoni mwa vivutio vikubwa ni Mazao ya Kimkakati yaTanzania katika soko la Italia na Barani Ulaya ambayo ni Parachichi, Korosho, Kahawa na Viungo.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 17 za Afrika zinazoshiriki Maonesho hayo kwa mafanikio makubwa sana.











