
Jumamosi 7/05/2922
WU®Media PRODUCTION LIMITED
Na Kagutta Maulidi
Rome Italy
Jumuiya ya Watanzania Rome,Jana wamesherehekea na kuadhimisha miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Sherehe hizo zimewajumuisha Watanzania kutoka mikoa mbalimbali ya Italy walioalikwa Kupitia Jumuiya zao.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy Mh Mahamoud Thabit Kombo, ambae aliongozana na mke wake Pamoja na vijana wao.
Sherehe zilianza kwa wimbo wa Taifa ulioimbwa na Watanzania wote wakiwa wamesimama kwa heshima ya Taifa, na baada ya wimbo wa Taifa Watanzania wakiongozwa na Balozi Mahamoud Thabit Kombo, walisimama Tena kwa dakika za kumbukumbu, heshima na Dua kwa WAASISI WA TAIFA wakiwemo wazee wote waliokuwepo katika tukio Hilo la miaka 58 iliyopita .
Baada ya heshima hizo kubwa, kulifuatiwa na Utambulisho wa viongozi Pamoja na Watanzania wengine walio hudhuria.
Utambulisho wa Maofisa na watumishi wa Ubalozi ulifanywa mkuu wa utawala wa Ubalozi Madam Jubilata Shao ambae nae pia aliongozana na mwenzi wake Pamoja na watoto . Na Mwisho Mh. Balozi alijitambulisha kwa wageni na kuitambulisha familia yake kwa ujumla. Pamoja na Watanzania pia waliokuwepo wageni Waitaliani ambao nao walioalikwa.
Katika ratiba muhimu iliyofuata, Mh Balozi Mahamoud Thabit Kombo alitoa historia fupi ya Muungano na kusisitiza umuhimu wa Watanzania kuijua historia ya Muungano na ya nchi yao kwa ujumla. Balozi aliwasisiza Watanzania kuhakikisha kuwa Watoto wenye asili ya Tanzania kuijua historia muhimu ya nchi yao. “Historia ya Muungano si rahisi kuihadithia kwa Muda mchache kwani ni ndefu na ya kusisimua “alisema Mh Balozi
Katika hotuba yake Mh Balozi pia alisema na kuelezea jinsi gani Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulivyo wa kipekee Sana Dunia kote na ni moja ya Muungano mkongwe,hivyo tuna Sababu za kuulinda na kujivunia kama Watanzania” alisema Mh Balozi.
Sherehe zilinogeshwa na msanii Binti mdogo wa KITANZANIA Dilamite ambae aliimba nyimbo nzuri Sana ambazo ziliwanyanyua Watanzania na kucheza kwa furaha.
Sherehe ziliendelea kwa kupata chakula,vinjwaji na mziki katika kufurahia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na baadae Ulifika wakati muhimu wa kukata keki kubwa ya Muungano iliyopambwa kwa nembo ya Taifa.

Mh Balozi Mahamoud Thabit Kombo amewataka na kuwashauri Diaspora, kufanya sherehe za Kitaifa kwa mzunguko wa kila MKOA kwani hiyo ni njia ya kujenga umoja na mshikamano baina yao,vile vile Balozi amewahakikishia Diaspora kuwa Ubalozi utaendelea kuwaunga mkono kwenye mambo yote yenye tija kwao na kwa Taifa.
Baada ya ratiba hiyo Mh Balozi aliwaaga na kuondoka huku akiwaacha Watanzania wakiendelea kufurahika.





























