0 0
Read Time:49 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

Watanzania wanaoishi mkoani , Emilia-Romagna wamesheherekea sikukuu mbili kwa pamoja, Pasaka na Eid El Fitri. Sikukuu hizi mbili kwa mwaka huu 2022 ziliongozana.

Katika sherehe hizo Watanzania hao wa Emilia-Romagna walitumia fursa ya mkusanyiko huo kutambulisha katiba mpya ya Jumuiya yao ya Modena “Centro Nord “ North ambayo inakwenda kusajiliwa baada ya kuwa wamesha chagua uongozi mpya.
Sherehe hizi zimefanyika siku ya jumamosi ya tarehe 7/05/2022,siku ambayo pia Jumuiya ya Watanzania Rome waliiandaa sherehe ya kumbukizi ya Miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambapo katika sherehe hiyo mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy, Mh.Mahmoud Thabit Kombo.


Katika Sherehe za Muungano, Mh. Balozi alituma salaam kwa Watanzania Modena, kwanza kuwatakia kila la heri katika sherehe Yao na kuwahakikishia kuwa yeye kama mlezi yupo Pamoja nao.

“Kitendo mlichofanya kusherekea kwa Pamoja sikukuu za Imani mbili za kidini,Mme dhihirishia dunia umoja na mshikamano wa Taifa letu” alisema Balozi Mahamoud Thabit Kombo.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %