0 0
Read Time:1 Minute, 54 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

MISHAHARA YAONGEZWA 23.3%

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Mayb14,2022.

Kabla ya wiki moja haijapita baada ya kuwapunguzia watanzania ukali wa maisha kupitia kupunguza tozo kwenye Nishati ya mafuta,Rais Samia Saluhu Hassan leo ameibuka na “package” nyingine tamu zaidi kwa watumishi wa umma Nchini!

“Package ya Mama” inaenda kuweka rekodi ya kwanza tangu Nchi ya Tanzania ipate uhuru wake kutoka kwa uwingereza mwaka 1961 kwa watumishi wa umma kuwahi kuongezewa mishahara kwa asilimia 23 baada ya miaka mitano ya “msoto” wa hatari!

Mama Samia anakuwa Rais wa pili ndani ya EAC baada ya Rais wa Congo kwa kutoa kiasi hiki kikubwa zaidi cha nyongeza ya mishahara ya watumishi wa umma ambacho mimi nimekibatiza kwa jina la “Package ya Mama”.

Rais Mama Samia anafanya haya huku Nchi ikiwa katika mkwamo mkubwa wa kupanda kwa bei za nishati ya mafuta duniani na Nchini lakini bado hakusita kugusa maisha ya watumishi wa umma Nchini!

Rais Samia anafanya haya huku kukiwa na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ambayo pia anaendelea kuitekeleza!Rais Samia hivi karibuni atakuwa anazindua ujenzi wa kipande cha reli ya SGR kutoka makotopora kwenda mkoani Tabora kuitekeleza ahadi na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020/25.

Hii ni ishara kuwa safari za mara kwa mara za nje za mama Samia zimempa ubavu wa kufanya mambo mengi ya kitaifa kwa mkupuo kitu ambacho labda kingekuwa kigumu kutekelezeka huko nyuma!Lazima tukubali kuwa safari za mama mpaka hapa zimemlipa na zimetulipa pia!

“…Tido,watu wangalie faida zinazotokana na safari hizi….”Mama Samia alinukuliwa katika mahojiano yake na Tido Mhando Mwandishi mkongwe wa habari Tanzania!

Hatua hii inamfanya Mama yetu Samia kuweza kuzima kelele zote zilikuwa zinaendelea mitandaoni zilizokuwa zinatoka kwa wapinzani wake!Jamaa safari hii watazima sigara!

Ni wazi kuwa hatua hii inaenda kuisukuma sekta binafsi nayo pia kuongeza mishahara ya wafanyakazi wao hivi karibuni hivyo watanzania kuweza kuimba wimbo mmoja!Hili litaenda sambamba pamoja na ongezeko la kibajeti katika kila sekta ikiwemo kilimo,maji,afya na sekta zingine!

Tuhudi hizo ni muendelezo wa Mh Samia kuendelea kujali maslahi ya umma baada ya mwaka uliopita kupunguza kodi katika mishahara hivyo kuongeza kipato cha wafanyakazi Nchini!

Hili ndilo “Jambo letu” ambalo Mama Samia alilowaambia!Mimi ni mjumbe tu,Mama Samia anasema eti, “Tukutane 2025 Kama Mnaweza”.

+255746726484.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %