0 0
Read Time:4 Minute, 24 Second

ATAJWA KUVUNJA REKODI. UCHAMBUZI WA TIJA 11 ZA WATUMISHI ZILIZOSHUGHULIKIWA

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

Anaaandika PhD Dkt.Ahmad Sovu

Awali ya yote napenda Niwasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kazi Iendelee.

Rais Samia Suluhu jana ametekeleza ahadi ya kuwapandishia mshahara wafanyakazi. Mshahara umeridhiwa kupanda kwa ongezeko la asilimia 23.3.
Hatua hii ya kupandisha mshahara kwa kiwango hiki imetajwa na wachambuzi kuwa haijawahi kutokea katika historia ya nchi hii.

Mathalan, ndugu Majid Mjengwa katika makala yake anasema kuwa;
Kupanda kwa asilimia 23.3 ni rekodi iliyowekwa na Rais Samia ambayo haijapata kushuhudiwa. Anaeleza kuwa hakumbuki ni lini Jamhuri iliwahi kupandisha mshahara kwa asilimia ya tarakimu mbili (Double digits) ambapo ameeleza kuwa hatua hii inairejesha shilingi mtaani.

Huyu ndiye Rais Samia Suluhu, ambaye amekuwa akionesha umahiri wa hali ya juu katika uongozi wake. Angeweza tu akatamka siku ile ya Mei mosi ila alitaka taratibu zifuatwe na ongezeko la mshahara liendane na hali ya uchumi.

Ambapo baada ya michakato yote muhimu anaridhia ongezeko la mshahara huo.

Itakumbukwa kuwa wakati Mheshimiwa Samia ametimiza mwaka 1 madarakani niliandika makala inayohusiana na uthabiti wa kauli zake katika hotuba na utekelezaji wa kauli hizo iliyochapishwa katika gazeti la Habari Leo. Kwa hakika kwa hili Mheshimiwa Samia ameendelea kudhihirisha uthabiti wa kauli zake.

Kwani, katika sherehe za Mei Mosi za mwaka 2021 kule jijini Mwanza aliahidi kuwa mwaka ujao, yaani mwaka huu wa 2022 atakuja na “package” nzuri ya kupandisha mishahara. Ilipofika tarehe hiyo Mheshimiwa Rais Samia akawaambia wafanyakazi kuwa ahadi yake atatimiza kama alivyosema Kwa sababu nshatoa ahadi mwaka jana, kwa hiyo nimeagiza jambo liwepo, mahesabu yanaendelea tutajua lipo kwa kiasi gani LAKINI JAMBO LIPO
Jana katika kutekeleza ahadi yake ya ulezi kweli jambo limekuwa Mheshimiwa Samia amepandisha mshahara kwa kiwango cha asilimia 23.3. Huyu ndio Rais Samia Suluhu Mthabiti wa kauli, kiongozi msikivu, mpatanishi, mfariji na mwenye huruma kwa watu wake.

Ufuatao ni uchambuzi wa tija au changamoto 11 zihusuzo wafanyakazi na namna alivyozishughulikia:

Mosi, kuongeza mshahara kwa asilimia 23.3 Mheshimiwa Rais ametekeleza ahadi hiyo jana. Ahadi hiyo imekuwa faraja kubwa sana kwa kila mfanyakazi na Watanzania wote. Hatua hiyo pia, imeelezwa kuwa itaongeza na kuchochea ukuaji wa uchumi na mzunguko wa biashara katika jamii.

Pia, imekuja wakati mwafaka kwani hali ya maisha imepanda hivyo itasaidia kupunguza makali ya maisha kwa wafanyakazi na wananchi kwa ujumla.

Aidha, hatua hiyo, itaongeza chachu, ari na bidii kwa wafanyakazi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Vilevile, hatua hii ya Mheshimiwa Rais Samia imetajwa kuja baada ya miaka 7 ya kutokupandishwa mshahara.

Fauka ya hayo, hatua hiyo imeelezwa kuwa ongezeko hilo la upandishaji wa mishahara lipo juu zaidi ukilinganisha na baadhi ya nchi jirani mwa Tanzania.

Ambapo kwa mujibu wa Blogu ya YonaPAVEA Kenya waliongeza kwa 12%, Uganda, Zambia na Rwanda chini ya 10% Huyu ndio Samia Suluhu Hassan.

Pili, Amepunguza kodi ya mshahara (payee) kutoka asilimia 9 hadi 8 Samia alipunguza kodi hiyo. Ambapo katika sherehe za Mei Mosi mwaka huu alieleza kuwa hatua hiyo imerejesha fedha zaidi kwa watumishi.

Tatu, Ameongeza ajira mpya 44,000 Mheshimiwa Rais Samia katika kuongeza tija kwa wafanyakazi ameongeza ajira 44 elfu ili kuimarisha ubora wa kazi na kukuza uchumi. Ajira mpya zilizotolewa zimetumia Shilingi Bilioni moja na milioni miamoja.

Nne, Kupandisha madaraja kwa watumishi 190,562 Mheshimiwa Samia amepandisha madaraja kwa watumishi mbalimbali ambao walikuwa hawajapandishwa kwa muda mrefu. Hatua hiyo ambayo aliifanya mapema tu baada ya kuwa Rais imechagiza kuboresha mazingira ya kiutendaji kwa wafanyakazi.

Tano, kulipa malimbikizo ya mshahara Mheshimiwa Rais Samia amelipa malimbikizo (arreas) kwa watumishi 75,000 ambapo serikali imetumia fedha jumla ya Shilingi Bilioni miamoja ishirini na nne na point 3 kutekeleza azma hiyo.

Sita, Kulipa mafao ya wastaafu kwa wakati Mheshimiwa Samia ameendelea kuleta faraja kwa wastaafu ambapo amesimamia kulipa mafao kwa wastaafu.

Saba, Kufuta tozo ya asilimia 6 ya Bodi ya mikopo ya elimu ya juu licha ya hiyo Mheshimiwa Rais Samia kuhusu elimu ya juu pia amefuta madeni chachefu yanayofikia Shilingi za Kitanzania Trilioni moja na Bilioni moja na sita ameyafuta. Kufutwa kwa madeni haya kumeongeza mzunguko na kurejeshwa fedha lukuki kwa wafanyakazi.

Nane, Kuongezwa kwa umri wa utengemezi wa mtoto kutoka miaka 18 hadi 21
Mheshimiwa Rais Samia ameongeza umri wa utegemezi ambapo jumla ya watoto 65,353 wametibiwa. Ambapo serikali imetumia Shilingi za Kitanzania Bilioni 3 na nukta 7 kulipia matibabu hayo.

Tisa, Marekebisho ya Sheria ya Bodi ya walimu
Mheshimiwa Samia amefanya marekebisho katika bodi ya walimu. Hali hiyo imesaidia kuleta tija kwa walimu.

Kumi, Ubadilishwaji wa kada miundo ya utumishi Ambapo watumishi 21,204 walifaidika. Serikali imetumia Shilingi za Kitanzania Bilioni 4 na pointi 3 kutekeleza azma hiyo.

Kumi na moja, Kupandisha vyeo watumishi 198, 215.
Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 41 kupandisha vyeo.

Hivi ndivyo ambavyo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametekeleza ahadi zake kwa vitendo na kuonesha uthabiti wa kauli zake. Kwa hakika mama ameleta faraja kwa watumishi Watanzania na Watanzania kwa ujumla.
Leo asubuhi nimeona baadhi ya arafa ni kama za kuchekesha lakini zinatoa picha ya faraja waliyoipata wafanyakazi wake. Moja ya ujumbe huo ulisema “walioko karibu na ikulu tunapenda kujua hali ya Rais wetu, ameamkaje? Kanywa chai?…😅😅😅. ” kwa hakika ni jambo la faraja.

Kongole sana Rais wetu, twakuombea siha Mola akutunze. Amina.

Mwandishi ni Mhadhiri na Mshititi wa Lugha
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere-Kigamboni DSM
0713400079

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %