0 0
Read Time:1 Minute, 39 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

TAKRIBANI WATOTO 19, WATU WAZIMA WAWILI WAUAWA KWENYE SHAMBULIO LA KIGAIDI KWENYE SHULE YA MSINGI MJINI TEXAS, MAREKANI.
Takriban watoto 19 na watu wazima wawili wameuawa na wachache kujeruhiwa katika shambulio la kigaidi katika shule ya msingi, huko Uvalde, Texas, Mei 24, 2022.

Kijana mmoja mzungu GAIDI amewauwa takriban watoto 19 na watu wazima wawili (Walimu) katika shule ya msingi katika jimbo la Texas nchini Marekani, maafisa walisema, katika shambulio baya zaidi la kupigwa risasi shuleni katika takriban muongo mmoja na ni moja katika matukio ya kutisha nchini Marekani, nchi inayokumbwa na msururu wa matukio ya watu kuuwawa kwa risasi.

GAIDI huyo alifyatua risasi katika Shule ya Msingi ya Robb – ambayo inasomesha watoto wenye umri wa miaka saba hadi 10 – katika jiji la Uvalde kabla ya kuuawa na vyombo vya sheria, maafisa walisema.

Gavana Greg Abbott alisema mmoja wa watu wazima wawili waliouawa alikuwa mwalimu. Maafisa wa serikali baadaye walithibitisha kwamba mtu mzima wa pili aliyeuawa pia alikuwa mwalimu.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumanne mchana, Abbott alisema gaidi huyo mwenye umri wa miaka 18 alifyatua risasi katika Shule ya Msingi ya Robb huko Uvalde, jamii ndogo iliyo umbali wa kilomita 80 (maili 50) magharibi mwa San Antonio.

Abbott alisema GAIDI huyo aliyetumia bunduki – ametambuliwa kwa jina la Salvador Ramos, mkazi wa Uvalde naye aliuawa na maafisa wa polisi kwenye eneo la tukio.

Matukio mengine ya KIGAIDI ya hivi karibuni ni pale mtu mmoja mwenye silaha aliposhambulia duka la vyakula katika mtaa wenye wakazi wengi Weusi wa Buffalo, New York, Mei 14, na kuuwa watu 10 huku wachunguzi wakasema ni uhalifu wa chuki za kibaguzi. Huko California wikendi iyo hiyo, mwanamume mmoja aliwafyatulia risasi waumini wa kanisa la Taiwan-Amerika, na kumuua mtu mmoja.

“Katika wiki mbili zilizopita, angalau watu 23 wamepoteza maisha yao katika tukio lingine la KIGAIDI, huko Buffalo, NY, na sasa Uvalde, Texas,” Meya wa Houston Sylvester Turner alisema katika taarifa yake.

Chanzo:
BBC: https://www.bbc.com/news/world-us-canada-61573377

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %