0 0
Read Time:1 Minute, 18 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

Na Mwandishi wetu

Zanzibar

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Uzinduzi wa Mwanamke Initiatives Foundation
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwasili katika hotel ya Golden Tulip air port Zanzibar kwa Uzinduzi wa Mwanamke Initiatives Foundation
Taasisi hiyo iliyozinduliwa ina lengo la kumsaidia mtoto wa Kike Shuleni pamoja na Watoto wengine ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao kielimu na kimaisha.
Rais Samia akikabidhi Tuzo kwa Mkurungenzi Mtendaji wa CRDB
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla pamoja na Mkewe Mama Sharifa Omar Khalfan wameshiriki katika uzinduzi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation uliofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Akitoa Salamu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hemed ameeleza kuwa SMZ inathamini juhudi zinazofanywa na Taasisi Binfasi katika kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kuwatumikia Wananchi wake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa Juhudi zinazofanywa na Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation ni za kupigiwa Mfano hasa kuunga mkono katika Sekta ya Elimu Nchini akitolea Mfano kufadhili vifaa kwa Skuli na Kambi za Wanafunzi wa Kidato cha Nne Mkoa wa Kusini Unguja katika kukuza ufaulu kwa Mkoa huo.
Aidha ameeleza kuwa miongozo ya Viongozi wakuu wa Nchi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi imesaidia kurahisisha ufanyaji kazi wa Taasisi Binafsi kwa kuinua wigo kwa Taasisi nyengine.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (AMPR)
19 Juni 2022

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %